Home Kitaifa Mwanza yaja na mikakati kabambe kupunguza migogoro ya Ardhi

Mwanza yaja na mikakati kabambe kupunguza migogoro ya Ardhi

Na Neema Kandoro Mwanza

WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetatua migogoro 945 na kutoa hati zaidi ya 1000 katika Halmashauri za wilaya nne Mkoani Mwanza kwa kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Disemba huku zoezi likiendelea kufanyika ngazi za kata.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Mwanza na Kamishina Msaidizi Mkoani hapa Happiness Mtutwa akisema kuwa wilaya ya Ilemela migogoro 243 ilitatuliwa huku Nyamagana migogoro 570 ilipata ufumbuzi huku utoaji wa Elimu ukipewa nafasi kwenye matukio hayo.

Aliendelea kusema kuwa katika wilaya ya Misungwi migogoro 106 ilipata ufumbuzi na Magu migogoro 26 imetatuliwa huku zoezi hilo likiendelea kufanyika kwenye eneo hilo.

Mtutwa alisema kutokana na hitaji la Serikali kuwataka kuwasogelea karibu wananchi Ili kuwatatulia wananchi kero zao wameanzisha Kliniki ya Ardhi ambayo imepata ufanisi katika maeneo waliyopita.

Alisema kuwa mwakani wanakusudia kutoa elimu kwa muda mrefu kwa watu wengi kwenye maeneo ambayo yatawezesha watu wengi kufika na yatajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali Ili kumaliza kero za ardhi kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!