Home Kitaifa WADAU WAKUTANA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TANGA YETU

WADAU WAKUTANA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TANGA YETU

Na Boniface Gideon, TANGA

WADAU wa Maendeleo Jiji la Tanga Leo wamekutana kwaajili ya kutathmini utekerezaji wa Miradi ya Tanga Yetu ambayo inaendelea kutekerezwa na ambayo imekwisha malizika pamoja na kuweka mikakati ambayo itasaidia kuboresha utekerezaji wa Miradi hiyo.

Tanga Yetu imefanikiwa kutekereza Miradi ya Maendeleo 17 yenye thamani ya Bil 7 ,Baadhi ya Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Bustani kubwa ya kapumziko Jijini Tanga maarufu Forodhani yenye thamani ya Bil 1.3 , Ujenzi wa mradi wa ufugaji kuku ambao mpaka mpaka Sasa umezarisha kuku 34,000 Wenye thamani ya zaidi ya mil 20, Ujenzi wa Kituo Cha Sayansi Cha STEM PARK pamoja na Kilimo Cha Mwani na ufugaji wa Majongoo Bahari kwa wakazi wa Mwambao wa Bahari.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amewataka Wadau wa Maendeleo pamoja na Wananchi wa Jiji la Tanga kuitunza Miradi ya Mbalimbali ya Maendeleo iliyojengwa na Taasisi ya Tanga Yetu chini ya ufadhili wa Botnar Foundation kwakushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga

Akizungumza Jana kwenye kikao cha tathmini utekerezaji wa Miradi ya Tanga Yetu kwa Wadau wa Maendeleo ya Jiji la Tanga,
Kaji Alisema Miradi hiyo ni mikubwa nakwamba Baada ya kumalizika itarudi chini ya usimamizi wa Serikali na Wananchi hivyo ni vyema Viongozi na wakazi wa Tanga wakabadilika fikra ,

“Tanga Bado tumelala na Wakati mwengine unajiuliza kwanini linaitwa Jiji ,hebu tuende kwa wenzetu tukajifunze kama mwanza ,hii Miradi ya Tanga Yetu inatakiwa tuitunze sisi wenyewe , Wadau wametusaidie Sasa sio kila kitu watufanyie ,hebu tuamkeni jamani”Alisisitiza Kaji

Aliwataka Madiwani kuwa wakali kwakuwaadhibu watendaji wazembe,

“Hapa tumeona Baadhi ya watendaji ni wazembe hasa Wahandisi Kuna Miradi mingi ya Halmashauri hasa Shule inasua sua ,Kuna Sehemu nimeenda nimekuta mirango ya Darasa ukiusukuma unaanguka wenyewe na Kuna Sehemu nimekuta Saruji imeganda haifanyiwi kazi ,Sasa nyie Madiwani Bado mnaishi nao watendaji wabovu kama hao”Alisema Kaji

Kwaupande wake Mwakilishi wa Botnar Foundation Nchini Tanzania ambaye pia ndio msimamizi Mkuu wa Miradi ya Tanga Yetu Dkt.Hassan Mshindo Alisema wamefanikiwa kuwafikia Vijana zaidi ya 100,000 ,

“Katika kipindi hiki kifupi tumefanikiwa kuwafikia Vijana nakuwabadilisha kuanzia kielimu Hadi kipato ambapo kwasasa kila kijana kipato chake kimepanda Hadi sh.100,000 kwa wiki ambapo hapo tuna mradi mkubwa wa kuku ambapo Hadi Sasa umezarisha kuku Wengi zaidi ya 30,000 Wenye thamani ya mil 20,000,000 na fedha zote hizo ni zao Vijana”Alisema Dkt.Hassani

Alisema katika Miradi ya Elimu imefanikiwa kuwafikia Vijana zaidi ya 2000 ambao walikuwa hawajui kusoma na kuandika lakini pia tumejenga Kituo Cha Sayansi Cha STEM PARK ambapo Hadi Sasa zaidi ya Vijana na Watoto 34,000 wameshanufaika”Alibainisha Dkt.Hassan

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!