
Na Boniface Gideon, Tanga
Waandishi wa habari wanawake kutoka vyombo mbalimbali mkoani Tanga leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Tanga ‘Bombo’, ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini.
Msaada huo umekabidhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo ili kuwasaidia watoto pamoja na akina mama wajawazito.

Katibu wa Waandishi wa Habari wanawake, Raisa Said, alisema msaada huo unahusisha sabuni na taulo za watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini, na kwamba una lengo la kuwasaidia wanawake pamoja na watoto.
Waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Tanga walipiga picha ya pamoja baada ya kutoka Hospitali ya Bombo kutoa msaada huo wa vitu mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho hayo mapema leo.








