Home Kitaifa SERIKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA MAJIKO BANIFU KWA ASILIMIA 80 KAGERA

SERIKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA MAJIKO BANIFU KWA ASILIMIA 80 KAGERA

Mradi wa usambazaji wa majiko banifu mkoani Kagera unalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, hali itakayosaidia kulinda afya za wananchi na mazingira.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa, Kanali Yahaya Ramadhani Kido, ambapo ameeleza kuwa matumizi ya majiko hayo yatapunguza magonjwa ya mfumo wa upumuaji yanayosababishwa na moshi, hasa kwa wanawake na watoto.

Aidha, Kanali Kido ameeleza kuwa mradi huo ni suluhisho la muda mrefu kwa changamoto za nishati ya kupikia, huku ukichangia kupunguza ukataji wa miti ovyo na uharibifu wa misitu pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Naye Mhandisi Mwandamizi kutoka REA, Deusdedith Malulu, ameeleza kuwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa unaolenga kufikisha matumizi ya nishati safi kwa asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2034, ambapo majiko 12,500 yatasambazwa mkoani Kagera.

Kupitia ruzuku ya Serikali ya asilimia 80, bei ya jiko imeshuka kutoka shilingi 100,000 hadi 12,450, hatua inayolenga kuwapa fursa wananchi wa kipato cha chini kumudu gharama na kuboresha maisha yao. Pia, viongozi wamehimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kununua majiko hayo ili kuboresha afya na kulinda mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!