Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bi. Zuhura Yunus pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Nishati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda pamoja na Viongozi Wakuu wa Taasisi za Serikali leo wamezungumza na Vyombo vya Habari kuhusu ziara ya Rais Samia nchini Oman pamoja na matokeo ya Filamu ya The Royal Tour katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es salaam leo June 28,2022.
Miongoni mwa yaliyosemwa ni ongezeko la Watalii na Ndege za Mashirika mbalimbali nchini baada ya Royal Tour “Baada ya Royal Tour Watalii wameongezeka na Wawekezaji wameongezeka sana, Watu wa Viwanja vya Ndege wanaangalia miruko ya ndege, kwa vipimo vyao inaonesha miruko imeongezeka na Wageni wanaofika Uwanja wa Dar es salaam wameongezeka”
“Ndege zinazofika nchini baada ya Royal Tour kwa taarifa ni kwamba Mashirika mengi yameongeza sana ndege zinazokuja, Fly Dubai zilikuwa ndege 10 sasa ndege 14 , Oman Air zilikuwa ndege mbili sasa ndege 7 kwa Wiki, Kenya Airways zilikuwa 19 sasa 22, Emirates zilikuwa 4 zinakwenda saba kwa wiki, Turkish Air zilikuwa 4 sasa zinakwenda saba” – Zuhura
“Wawekezaji wameongezeka hasa kutoka Marekani na kuna Mwekezaji mkubwa anataka kuwekeza Serengeti, Arusha, Ngorongoro Mwanza na Dar esalaam anataka kujenga Mahoteli” – Zuhura