Home Kitaifa WAZIRI UMMY: IPO HAJA YA KUANGALIA NAMNA YA KUTOA HUDUMA ZA KISAIKOLOJIA...

WAZIRI UMMY: IPO HAJA YA KUANGALIA NAMNA YA KUTOA HUDUMA ZA KISAIKOLOJIA NA AFYA YA AKILI

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea nchini, ipo haja ya kuangalia namna ya kutoa huduma za kisaikolojia na afya ya akili.

Kando na hilo ameshauri kuangaliwa uwezekano wa kuwa na vituo vya ushauri wa kisaikolojia ili kuwaepusha vijana wengi kutumbukia kwenye sonona.

Ummy ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 10, 2022 wakati wa kongamano la kwanza la kitaifa la afya ya akili linalofanyika mkoani Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya afya ya akili.

Waziri huyo amewataka wadau kutumia kongamano hilo kutoa maoni ya nini kifanyike kukabiliana na changamoto ya afya ya akili ambayo imekuwa tatizo kubwa kwenye jamii.

Kutokana ukubwa wa tatizo hili hebu tuangalie kwanini tusiangalie uwezekano wa huduma za ushauri wa kisaikolijia na huduma za matibabu zipatikane kwenye bima ya afya.”

Nataka tutoke hapa tukiwa na mawazo yanayoweza kufanyiwa kazi tukapata matokeo chanya, upande wetu Serikali tunalichukulia suala hili kwa uzito mkubwa ndiyo sababu suala hili tumeliweka kwenye mpango,” amesema.

Ummy amesema kuanzia sasa mpango wa taifa wa magonjwa yasiyoambukiza utafahamika kama mpango wa Taifa wa magonjwa yasiyoambukiza, afya ya akili na ajali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!