Home Kitaifa WAZIRI KAIRUKI ATOA MAAGIZO KWA WAKALA WA MABASI YAENDAYO KWA HARAKA (DART)

WAZIRI KAIRUKI ATOA MAAGIZO KWA WAKALA WA MABASI YAENDAYO KWA HARAKA (DART)

Angela Msimbira OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki ameutaka Walaka wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART) kurudi na kupitia nauli za mabasi ili ziwe zinazohimilika kwa wananchi wa vipato vyote.

Kairuki ameyasema hayo leo Oktoba 10, 2022 wakati akizungumza na watumishi wa DART wakati wa ziara ya kikazi katika taasisi hiyo ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema DART inapaswa kuhakikisha kuna kuwa na huduma ya usafiri ambayo inahimilika kwa wananchi wenye vipato vya aina zote.

Sisemi bei zifutwe, sisemi pia bei ziwe kiasi gani, lakini wataalamu warudi waangalia kwa jicho la kibiashara lakini wakati huo huo jicho la wananchi.”amesema Waziri Kairuki

Waziri Kairuki pia ameipongeza DART Kwa kuja na mpango wa kuongeza mabasi 177 yanayotumia gesi asilia sambamba na kumpongeza hatua ya kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 37.16 baada ya kukusanya Sh bilioni 10.8 katika robo ya kwanza ya mwaka.

Aidha, Waziri Kairuki ameagiza kuipitia mikataba ya ubia ya uendeshaji mabasi kwa kuangalia vifungu vinavyohitaji utekelezaji ili utekelezaji ufanyike kwa wakati.

Kuhusu ujenzi wa miundombinu, Waziri Kairuki amewataka kuhakikisha wanakuwa ndani ya wakati huku akipongeza utekelezaji wa awamu ya pili ambayo imefikia asilimia 66.

Waziri Kairuki amemshukuru Rais Samia kutoa Sh bilioni 7.8 kwa ajili ya karakana na kuutaka uongozi kuhakikisha inafuata sheria katika kufanya tathmini na kulipa fidia kwa wakati.

Aidha ameihimiza DART kuendelea kutumia mifumo na teknolojia katika utendaji kazi wa Wakala na utoaji huduma kwa kuangalia mifumo ambayo itatoa unafuu wa gharama kwa kiasi kikubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!