Home Kitaifa WAZIRI SHEMDOE: FANYENI KAZI KWA WELEDI KUWALATEA WANANCHI TABASAMU

WAZIRI SHEMDOE: FANYENI KAZI KWA WELEDI KUWALATEA WANANCHI TABASAMU

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki  Shemdoe,akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI  uliofanyika leo  Machi 26, 2026 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki  Shemdoe,akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI  uliofanyika leo  Machi 26, 2026 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki  Shemdoe (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI  uliofanyika leo  Machi 26, 2026 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki  Shemdoe (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI  uliofanyika leo  Machi 26, 2026 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki  Shemdoe (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI  uliofanyika leo  Machi 26, 2026 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki  Shemdoe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua   Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI  uliofanyika leo  Machi 26, 2026 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Mzalendo blog-DODOMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki  Shemdoe, amewataka watumishi wa ofisi hiyo kufanya kazi kwa weledi, bidii na ubunifu ili kuongeza tija na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI  uliofanyika leo  Machi 26, 2026 jijini Dodoma Waziri Shemdoe amesema kuwa baraza hilo ni jukwaa muhimu la kuimarisha ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi katika kufanikisha majukumu ya taasisi.

Amesema mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kujadili masuala ya msingi mahali pa kazi, ikiwemo migogoro, maslahi ya watumishi na kuboresha mazingira ya kazi, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia haki, wajibu na maadili ya utumishi wa umma.

 “Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI ina jukumu kubwa la kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika ngazi mbalimbali za utawala, kuanzia mikoa, wilaya hadi vijiji, hivyo ni lazima watumishi wake wawe na mshikamano na nidhamu ya kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.”amesema Prof.Shemdoe

Aidha, amewataka wajumbe wa baraza hilo kutumia vikao vyao kujadili mipango na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 kwa kuzingatia vipaumbele vya taasisi, huku akibainisha kuwa usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa mipango hiyo ni muhimu katika kufikia malengo yaliyowekwa.

Amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya na elimu, ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri pamoja na uendelezaji wa mifumo ya TEHAMA, huku akitaja changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa fedha za maendeleo, ufinyu wa bajeti na uhaba wa watumishi katika baadhi ya sekta.

Hata hivyo, amewataka watumishi kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto hizo na kuzingatia afya zao kwa kushiriki michezo na kufanya mazoezi, kabla ya kutangaza rasmi ufunguzi wa mkutano huo na kuwatakia wajumbe majadiliano yenye mafanikio.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI,Adolf  Ndunguru,ameeleza kuwa Mabaraza ya Wafanyakazi ni vyombo vya kisheria vinavyolenga kuongeza tija, uwajibikaji na kutoa fursa kwa watumishi kujadili masuala muhimu yanayohusu utendaji na maslahi yao.

Amebainisha kuwa baraza hilo ni jukwaa muhimu linaloleta pamoja uongozi na watumishi ili kujenga utamaduni wa ushirikiano, nidhamu ya kazi na ufanisi katika taasisi.

 “Mkutano huo utajadili mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, akieleza kuwa utekelezaji wake utasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo. Alisisitiza utayari wa watumishi kupokea maelekezo ya Waziri ili kuboresha utendaji na kufikia malengo ya Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.”amesema Ndunguru

Hata hivyo amemshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kueleza kuwa uwepo wake ni ishara ya dhamira ya kuimarisha utendaji kazi na kusikiliza watumishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!