Home Kitaifa WAZIRI MABULA ATAKA HATUA ZA KINIDHAMU ZICHUKULIWE KWA WATUMISHI WASIO NA...

WAZIRI MABULA ATAKA HATUA ZA KINIDHAMU ZICHUKULIWE KWA WATUMISHI WASIO NA NIDHAMU

Na Magreth Mbinga

Watumishi wa umma wametakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ambapo kumekuwa na kutoheshimiana baina ya viongozi na wanaowaongoza pamoja na kuogopa kubeba dhamana kama kiongozi kwa kukwepa lawama .

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Anjelina Mabula wakati wa kufungua kikao kazi kilichowashirikisha Makamishna wa Mikoa yote ili kujadili utendaji kazi wa Wizara hiyo.

Pia Dk Mabula amewataka watendaji kutekeleza majukumu waliyopewa ambayo yapo kisheria ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea kama Wizara katika kutekeleza majukumu yake.

“Ninatambua wazi Katibu Mkuu hili umelizungumza sana tangu ulipofika Wizarani na Mimi nikushukuru kwamba kwa kipindi hiki kifupi ulichokaa umeifahamu Wizara vizuri na ndio maana maelekezo yako unayotoa kwa watumishi nimeanza kuona matokeo ya utendaji kazi”amesema Dk Mabula.

Sanjari na hayo Dk Mabula amesema pamoja na utendaji mzuri wa watumishi lakini kumekuwa na tatizo katika baadhi ya Mikoa na Halmashauri ambazo Makamishna wasaidizi wanazisimamia hakuna muunganiko ambapo inasababisha malalamiko kwa Wananchi ambayo kinyume cha matarajio ya Wizara.

“Nimetoa maelekezo ambayo natakiwa nipatiwe taarifa haraka na kufanyiwa kaxi kwenye eneo hili sijaona uharaka na uthabiti ambao unatakiwa katika kutekeleza maagizo niliyoyatoa ,niliagiza ufanyike uhakiki wa mashamba yote na viwanja ambavyo vimetelekezwa na nilitaka taarifa hii niipate julai 30 mpaka sasa ni mikoa 17 ambayo imewasilisha”amesema Dk Mabula.
Vilevile Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Allan Kijazi ametoa mapendekezo ambayo yatajadiliwa kwenye kikao kazi hiko na kutaka watoke na mkakati wa kutatua migogoro ambayo ipo.

“Timekutana na wadau kuanzia ngazi ya chini hadi juu na eneo kubwa ni kulalamikiwa kwa watendaji ambapo wanatoa huduma kwa kumfahamu mtu kama mtu anataka huduma na hakuna unaemfahamu hatapata “amesema Dk Kijazi.

Dk Kijazi alimalizia kwa kuwataka watumishi kujua wajibu wao wa kutatua migogoro ili kufikia malengo ya mkakati ambao wamejiwekea kama Wizara .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!