Home Kitaifa WAZIRI AWESO AHIMIZA TANGA-UWASA KUBAKI KWENYE UBORA WAKE

WAZIRI AWESO AHIMIZA TANGA-UWASA KUBAKI KWENYE UBORA WAKE

Na.Boniface Gideon,

TANGA

Waziri wa Maji mh.Jumaa Aweso ameitaka bodi mpya ya Mamlaka ya maji Tanga-Uwasa kuhakikisha mamlaka hiyo inasonga mbele kwa kuweza kuendelea kubaki kwenye ubora wake ya kuongoza kuwa mamlaka bora nchini.

Haya aliyasema wakati akizindua bodi hiyo katika hafla ya kuwaaga wajumbe wa bodi inayomaliza muda wake iliyofanyika katika viwanja vya ofisi za mamlaka hiyo ambapo alisisitiza wajumbe na viongozi kufanya kazi kwa weledi ili waaminike zaidi kulinda nafazi zao.

Aliongeza kusema kuwa kipimo cha kwanza kuonyesha ubunifu wa viongozi katika kutekeleza wajibu kwa wakati kwa kusimamia miradi ya maji inakamilika kama ilivyopangwa ili wananchi wapate maji safi na salama na ya kutosheleza.

“Dhamira na ilani ya serikali ni kuhakikisha ifikapo 2025 upatikanaji wa maji uwe umefikia asilimi 95 katika utekelezaji lakini kwa mamlaka ya maji Tanga uwasa mpaka sasa tayari mmeshafikia aslimia 96 ya utekelezaji hivyo mnatakiwa kuendelea kuhakikisha kubaki kwenye ubora huo ili miradi ya mikakati itakapo kamilika wafikie alisimia 100.alisema Aweso

Sambamba na hayo alimshukuru Rais Samia Suluh Hassan kwa kutoa Dola milioni 500 kwa ajili ya miradi ya kimkakati ambao imetolewa kwa ajili miji 28 hapa nchini ambapo kwa mkoa wa Tanga imepatikana shilingi bilioni 190 kwa ajili miji mine .

Aidha aliwakumbusha watumishi wa Tanga Uwasa kuweza kuwa na tabia ya kuwahudumia wananchi na kuwasikiliza kwa kuwahudumia ipasavyo ili kuondokana na malalamiko yasiyo ya lazima.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso aaliwapandisha vyeo watumishi wawili wa mamlaka hiyo na kuwa wagurugenzi wa mamlaka za maji ambao wanasubiri kupangiwa vituo vyao vya kazi watumishi hao ni aliyekuwa mhandishi wa mamlaka Rashidi Mwinjuma na Dora Killo ambaye pia alikuwa mtumishi wa mamlaka hiyo.

Kwa upande wa aliyekuwa mstahiki Meya wa jiji la Tanga na mjumbe bodi iliyomaliza muda wake , Mustapha Selebosi alisema kuwa bodi hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira ,Tanga Uwasa ilikuwa ikifanikiwa kutenga kiasi cha fedha sh. Bilioni 4 kila mwaka katika mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga miundo mbinu na masuala jamii.

Sambamba hayo alieleza changamoto kubwa walikuwa nayo wakati wa uongozi wao ni pamoja na Mamlaka hiyo kuwa na chanzo kimoja cha maji katika kituo kikuu cha bwawa la maji Mabayani, “ ambayo kutokana na ongezeko kubwa la watu na mabadiliko ya tabia ya nchi imesababisha upungufu wa maji katika baadhi ya maeneo hivyo namba wewe kama waziri mwenye dhamana tanaomba utusaidie kuongeza bajeti kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundo mbinu na utunzaji mazingira katika vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja kuapata chanzo kingine ili kuweza kupata maji ya kutosheleza” .alisema selebosi.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!