Na Lookman Miraji.
Kampuni ya mtandao wa mawasiliano nchini ya Airtel imezindua rasmi kampeni mpya ambayo itawanufaisha watumiaji wa mtandao huo hapa nchini.
Kampeni hiyo ijulikanayo kama “Jiboost” imezinduliwa rasmi leo hii katika makao makuu ya mtandao huo yalioko Kinondoni, dar es salaam.
Akizungumza leo hii mkurugenzi wa mtandao airtel money Andrew Rugambo ameelezea kampeni hiyo huku akionekana kufurahishwa na ujio wa kampeni hiyo.
“Tunafurahia kutambulisha kampeni ya jiboost na Airtel money ikiwa ni sehemu ya kujitolea kufikisha thamani kwa wateja wetu. Promosheni hii imeundwa ili kuwazawadia wateja kwa kutumia airtel money katika maisha yao ya kila siku , iwe ni kununua saa za maongezi, kununua vifurushi au kufanya malipo ya bili pamoja na huduma za kiserikali ,katika kila muamala unaofanya watumiaji wetu kuwa karibu zaidi na kupata super bonus na pia tunajivunia kuwa mstari katika suluhisho la ubunifu wa pesa za miamala.” Alisema hayo mkurugenzi huyo.
Kampeni hiyo itakuwa ikiendeshwa kwa muda wa miezi mitatu ambapo watumiaji watapata bonasi za nyongeza mpaka kufikia kiasi cha shilingi elfu ishirini endapo utakapojiunga na mtandao huo au kutumia huduma za airtel money.