Home Kitaifa DC CHIKOKA AMSHUKURU RAIS DKT.SAMIA KULING’ARISHA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI KWA TAA...

DC CHIKOKA AMSHUKURU RAIS DKT.SAMIA KULING’ARISHA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI KWA TAA ZA BARABARANI

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuling’arisha jimbo la Musoma vijijini kwa mwanga wa taa za barabarani.

Shukrani hizo amezitoa jana septemba 25 mara baada ya kukitembelea usiku Kijiji cha Suguti kilichopo kwenye jimbo hilo.

Amesema kufungwa na kuwashwa taa za barabarani kumewezesha wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi hadi usiku.

Amesema Rais Dkt.Samia ameendelea kufanya kazi kubwa katika kuhakikisha wananchi mjini na vijijini wanafanya shughuli za kiuchumi mchana na usiku kwa usalama.

Chikoka amesema wananchi wa Kata na Kijiji cha Suguti wameonyesha furaha kwa kupata mwanga wa taa barabarani na kufanya biashara hadi usiku.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema hilo ni jambo kubwa lililofanywa na Rais Dkt.Samia na sio la kuacha kushukuru.

” Hapa sio daraja la Tanzanite jijini Dar es salam bali ni Kijiji cha Suguti jimbo la Musoma vijijini limeng’aa na kuwaka.

” Sasa wananchi wanafanya shughuli zao za kiuchumi mchana hadi usiku kwa raha na amani wakiwa na mwanga ndio maana tunamshukuru Mama Samia”,amesema.

Chikoka amemshukuru pia mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa ufatiliaji wake na kuhakikisha maendeleo yanaendelea kuonekana jimboni

Adha ametoa pongezi kwa Tanroads mkoa wa Mara kwa kuweka na kuwasha taa hizo na kutoa wito kwa wananchi kuwa waangalizi na kuzilinda ili kuendelea kuwapa mwanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!