Na Magreth Mbinga
Wakati zikiendelea hatua za mwisho kabla ya kuanza safari za treni ya kisasa SGR wataalamu kutoka shirika la Reli Korea Kusini (KORAIL) wamewasili nchin Kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uendeshaji wa reli Hiyo.
Akizungumzaa na waandish wa habari mkurugenzi mtendaji wa TRC Mhandisi Masanja Kadogosa, amesema mafunzo hayo yatakuwa kwa nadharia na vitendo yatakayotolewa kwa watumishi wa shirika la reli Tanzania TRC ambao watahusika katika uendeshaji wa reli Katika maeneo mbalimbali.
“Watachukuliwa baadhi ya vijana wa lika mbalimbali ambao watajifunza kutumia reli hii ya kisasa lengo ni kupata wataalamu wa ndani ya Nchi kutokea hapa shirika la reli TRC ambao watasaidia Taifa na kuepuka ghara ya kuajiri wataalamu kutoka nje “amesema Mhandisi Kadogosa.
Kwa upande wake meneja wa uendeshaji na matengenezo wa KORAIL,Soung Yong Lee amesema timu yake iko tayar kutoa utaalamu walionao, katika uendeshaaji wa reli ya SGR kutokana na uzoefu wa shirika hilo kwenye usafiri huo.