Home Kitaifa WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

Na. WAF, Dodoma

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewaasa wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya Ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa kutokea katika Nchi jirani ya Uganda.

Dkt. Mollel amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma na kutoa tahadhari hiyo huku akiwataka wananchi kuepuka safari zisizo kuwa za lazima kwenda maeneo ambayo yameripotiwa kutokea ugonjwa huo.

Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya tayari imeshatoa maelekezo kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufanya ufuatiliaji zaidi mipakani kabla ya wananchi kuingia na kutoka nchini.

Mara nyingi tumekuwa tukiangalia tuu UVIKO-19, hata pale uwanja wa ndege sasa tuangalie na haya magonjwa mengine yanayotokea” amesema Naibu Waziri Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel amewatoa hofu wananchi na kusema kuwa Tanzania bado ni salama na hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini kuugua ugonjwa wa Ebola.

Bado nchi yetu ni salama tunawaomba wananchi mshirikiane na Serikali kujilinda na tufuate maelekezo yanayotolewa na Serikali pamoja na namna ya kujikinga” amesema Dkt. Mollel

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!