Home Kitaifa RC MAKALLA ARIDHISHWA NA HALI YA MAJI RUVU JUU NA CHINI.

RC MAKALLA ARIDHISHWA NA HALI YA MAJI RUVU JUU NA CHINI.

  • Atoa wito Kwa Wananchi kulinda vyanzo vya maji Na kuombea mvua Za Vuli zinyeshe ili maji yasipungue.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewahakikishia Wakazi wa Mkoa huo kuwa Hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji Safi ni nzuri Kufuatia DAWASA kuchukuwa hatua stahiki za kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji msimu wa kiangazi ikiwemo Ujenzi wa Mabwawa ya kutunza Maji.

RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara kwenye Vyanzo vya Maji Ruvu juu na Chini akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge pamoja na wajumbe wa Kamati za ulinzi na usalama za Mkoa wa Dar es salaam na Pwani.

Katika ziara hiyo RC Makalla amejionea kina Cha Maji Ruvu juu kikiwa Mita 16 na Ruvu Chini Mita 4.2 Ambapo kwa mujibu wa DAWASA kiwango Cha Maji Cha Sasa kinaweza kutuvusha salama kipindi Cha Kiangazi.

Kutokana na Hali ya upatikanaji wa Maji kuwa ya kuridhisha RC Makalla ameelekeza Kamati ya Ulinzi na usalama na Mamlaka ya Bonde la Wami/Ruvu kufanya Operesheni za Mara kwa mara na kuwachukulia hatua watu watakaobainika kuchepusha maji bila Vibali.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi wa Dini kufanya Dua za kuombea mvua za Vuli zinyeshe ili yasitokee majanga ya ukame Kama yaliyotokea mwaka Jana.

Pamoja na hayo RC Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitiada za dhati anazofanya kuboresha sekta ya Maji kupitia miradi Mikubwa ya usambazaji wa maji pembezoni Mwa mji na kuwapongeza DAWASA kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kusimamia Vizuri miradi ya maji.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DAWASA Eng. Cyprian Luhemeja amesema Mamlaka hiyo inaendelea kufanya kila jitihada za kuhakikisha kiasi Cha Maji kilichopo kinalindwa na kudhibiti upotevu wa maji.

Aidha Eng. Luhemeja amewataka Wananchi kutunza na kulinda Vyanzo vya Maji ili kuwepo na upatikanaji wa maji ya uhakika.

Itakumbukwa kuwa mnamo mwaka Jana maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam yalikumbwa na tatizo la uhaba wa maji Kutokana na ukame uliosababishwa na kutokunyesha kwa mvua za Vuli na ndio maana siku ya Leo Wakuu wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani pamoja na Kamati za ulinzi na usalama wameona ni vyema kuchukuwa hatua za kukabiliana na Changamoto hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!