Home Kitaifa RAIS SAMIA APONGEZA UFAULU SHULE ZA JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA

RAIS SAMIA APONGEZA UFAULU SHULE ZA JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza Wakuu wa Shule zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM Tanzania, kwa matokeo mazuri ya mitihani ya kidato cha sita kwa kuondoa alama sifuri.

Katibu Mkuu Ndugu Daniel Chongolo leo tarehe 15 Julai, 2022 wakati akifungua kikao cha wakuu wa shule za sekondari zinazomilikiwa na jumuiya hiyo chenye lengo la kujadili mwenendo wa shule za Chama na namna ya kuboresha taaluma ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa salamu za Mwenyekiti wa Chama.

Ndugu Chongolo amesema Rais Samia alipoelezwa kuhusu kikao hicho cha walimu wakuu wa shule za jumuiya alihoji maendeleo ya shule hizo.

Nilipomueleza (Samia) kuhusu matokeo ya mitihani ya kidato cha sita akaniuliza shule za jumuiya zinaendeleaje, nikamwambia mambo ni mazuri, hazina alama za mwisho”.

Nikamwambia asilimia 80 hadi 90 ya wanafunzi waliofanya mtihani wamepata alama za daraja la kwanza, pili na wachache la tatu, akasema angekuja Dodoma kuwapongeza kama angekuwepo,” alisema.

Katibu Mkuu ameongeza, ”Amenituma kuwaambia kuwa anawapongeza kwa kazi nzuri na kubwa mliyofanya ya kufanikisha matokeo haya”.

Akizungumza na Walimu hao, Ndugu Chongolo amewapongeza walimu hao kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuondoa alama sifuri na kuwezesha wanafunzi wawili wa michepuo ya Sayansi (PCB & PCM) wa shule hizo kuingia nafasi kumi bora akieleza kama walimu hao wangekuwa sekta ya afya wangekuwa madaktari bingwa.

Amesisitiza kuwa shule hizo zilianzishwa kwa lengo la kuongeza wigo wa utoaji elimu kwa wanaokosa fursa kwenye machaguo ya shule za sekondari, wanaotamani kuendelea lakini hawakufanya vizuri.

Ndugu Chongolo ameongeza kuwa, mpaka sasa kazi haijaisha lakini ipo nyingine ya ziada kwakuwa bado lengo la shule kuwezesha vijana kupata fursa ya elimu bora ili kuendeleza ndoto ya kuendelea na masomo upo palepale.

Aidha, Katibu Mkuu aliwataka walimu hao kujenga nidhamu ili wasigeuze maeneo ya kazi kuwa ya migogoro na badala yake wakaze buti ili kasi hii iliyopo mwaka mmoja ujao kuwepo wanafunzi wengi hadi kukosa nafasi kwenye shule hizo.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kueleza namna Serikali ya awamu ya Sita ilivyoweka mkazo katika kuwasaidia vijana wanaotoka katika familia maskini kwa kuongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 bajeti imeongezeka kufikia Shilingi bilioni 573 ambapo wanafunzi wanufaika wataongezeka kutoka 177, 8800 mpaka 205, 500.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!