Home Kitaifa NAIBU WAZIRI WANU AWASILISHA RANDAMA ZA BAJETI 2026/2027 BUNGENI

NAIBU WAZIRI WANU AWASILISHA RANDAMA ZA BAJETI 2026/2027 BUNGENI

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidhi Ameir, leo Mei 6, 2026, amewasilisha Bungeni jijini Dodoma randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa niaba ya Waziri wa Elimu.

Uwasilishaji huo ni hatua ya awali kuelekea hotuba rasmi ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inayotarajiwa kuwasilishwa kesho bungeni, ambapo mwelekeo wa sekta ya elimu kwa mwaka ujao wa fedha utawekwa wazi.

Katika mwaka wa fedha 2025/2026, wizara hiyo iliomba na kuidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 2.44 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu, kuongeza ubora wa ufundishaji pamoja na kuimarisha tafiti na ubunifu.

Swali linalobaki ni je, mwaka huu Wizara ya Elimu itaomba kiasi gani—na je, kitaendana na matarajio ya kuboresha zaidi sekta ya elimu nchini?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!