Home Kitaifa MHE.SAMIA-AKEMEA UHARIBIFU VYANZO VYA MAJI.

MHE.SAMIA-AKEMEA UHARIBIFU VYANZO VYA MAJI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa maji wa Shongo-Mbalizi, mkoani Mbeya na kuwataka wananchi kulinda mazingira, pamoja na vyanzo vya maji.

Mhe. Rais akiongea na wakazi wa Mbalizi amesema serikali inaweka fedha nyingi katika miradi ya maji ili wananchi wapate huduma ya majisafi, na hivi sasa wananchi wameona hali ya tofauti ya huduma ya maji awali kabla ya mradi na sasa ambapo maji yanapatikana kwa asilimia 95.

“Yeyote atakayeharibu chanzo cha maji achukuliwe hatua stahiki” Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema na kuongeza ni wajibu wa viongozi na wananchi kulinda vyanzo vya maji ili miradi itoe huduma ya maji wakati wote.

Ameagiza maji yanapokatika kutokana na dosari yoyote wananchi wapewe taarifa mapema na sio watendaji kukaa kimya bila kueleza kinachoendelea katika huduma ya maji.

Awali akiongea katika hafla hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema mradi huo utahudumia wakazi wapatao elfu 80 na unazalisha lita milioni 8.1 kwa siku.

Wananchi watakaonufaikana na mradi huu mkubwa ni kutoka maeneo ya Mbalizi, Nsalala, Songwe, Mlima wa Reli, Mapelele, Izumbwe na Jeshini na kutoa fursa kwa wananchi wa maeneo hayo kutumia muda wa kutosha kufanya shuguli za kiuchumi badala ya kutafuta maji.

Wizara ya Maji imefanya utekelezaji wa mradi huu kwa miezi 12 kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya WSSA), kwa thamani ya shilingi bilioni 3.3 ikiwa ni sehemu ya kuzidi kuimarisha huduma za majisafi nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!