Home Kitaifa WAGONJWA WA AFYA YA AKILI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 13 DUNIANI

WAGONJWA WA AFYA YA AKILI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 13 DUNIANI

Na WAF – DSM

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Rehema Madenge amesema kuwa, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), katika kipindi cha muongo mmoja uliopita kumekuwa na ongezeko la takribani asilimia 13 la wagonjwa wa akili.

Bi. Rehema Madenge ameyasema hayo, katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya afya ya akili Duniani yaliyofanyika leo Oktoba 3, 2022 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, yenye kauli mbiu ya “Afya ya akili ni kipaumbele kwa wote.”

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), katika kipindi cha muongo mmoja uliopita kumekuwa na ongezeko la takribani asilimia 13 la wagonjwa wa akili.” Amesema, Bi. Rehema Madenge.

Amendelea kusema kuwa, inakadiriwa kuwa na wagonjwa milioni 7 wenye magonjwa mbalimbali ya akili na matumizi ya dawa za kulevya nchini, huku miongoni mwao zaidi ya watu milioni1.5 wanaishi na ugonjwa wa Sonona (Depression).

Sambamba na hilo, ameweka wazi kuwa, kumekuwa na matukio mengi ya ukatili ambapo wanawake wanne kati ya kumi walio katika umri wa miaka 15 – 49 walifanyiwa ukatili wa kimwili, wakati takribani wanawake wawili kati ya kumi walifanyiwa ukatili wa kingono, hii hutokana na ongezeko la magonjwa ya akili.

Aidha, amesema sababu kubwa ya matatizo ya Afya ya akili ni mabadiliko katika mfumo wa malezi ndani ya familia na jamii, msongo wa mawazo na matumizi ya vilevi kupita kiasi hususani pombe, bangi na dawa nyingine za kulevya.

Sababu kubwa ya matatizo ya Afya ya Akili ni mabadiliko katika mfumo wa malezi ndani ya familia na jamii, msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa kushindwa kuhimili mahitaji ya kila siku, na matumizi ya vilevi hususani pombe, bangi na dawa nyingine za kulevya.”Amesema.

Sambamba na hilo, ametoa wito kwa Wananchi kusaidia wahusika wa matatizo ya afya ya akili kupata matibabu, huku akisisitiza kuepuka unyanyapaa na kuwatenga wagonjwa wa hao ili kuwasaidia kurudi katika hali ya kawaida.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema, Mpaka sasa, huduma za afya ya akili zinaendelea kutolewa katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya vya umma na vya binafsi Jijini Dar es Salaam.

Aliendelea kusisitiza kuwa, huduma hizi ziantolewa kwa kutumia Wataalamu wabobezi katika utoaji wa huduma za afya ya akili, lakini katika vituo ambavyo havina wabobezi wa afya ya akili, watoa huduma wengine wamekuwa wakijengewa uwezo ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na huduma hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasiyoambukiza Wizara ya Afya Dkt. James Kiologwe amesema, takwimu kutoka vituo vya kutolea huduma za afya ya mwaka 2019/20 hapa nchini zinaonyesha kuwa, takribani wagonjwa 711,789 sawa na asilimia 10 tu ya wagojwa milioni 7 wamepatiwa huduma za afya ya akili na kukiri kuwa, dadi hii ndogo ya mahudhurio inachangiwa na uelewa mdogo wa jamii kuhusiana na matatizo mbalimbali ya afya ya akili na unyanyapaa.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!