Home Kitaifa WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTETEA HAKI ZAO

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTETEA HAKI ZAO

NA Magreth Mbinga

Waandishi wa habari wanapata shida nyingi bila kujua kwamba nawao wanatakiwa kutetea haki zao ndio maana Jukwaa la Wahariri Tanzania limekaa na kuona ipo haja ya mwandishi wa habari kujua anahitaji kujitetea pia.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Ndugu Deodatus Balile katika mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Jukwaa hilo yaliyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari na Wahariri kutetea Haki zao .

Ndg Balile amesema kwa kujua matatizo ambayo wanahabari wanakabiliana nayo watajua namna ya kuyatetea na itaifanya Dunia ijitambue na wakiondoa kasumba ya kutoandika habari ambazo zinawahusu itasaidia wanahabari kuwa katika hali nzuri.

“Vyombo vya habari vinafanya kazi ya kujenga uelewa katika jamii kuwafanya wananchi kufanya uamuzi kutokana na uelewa walionao na demokrasia itakua watafanya uamuzi wa kumchagua Fulani so kwasababu amempatia kitu bali ameahidi kufanya mambo ya msingi katika jamii” amesema Balile.

Pia Balile amesema vyombo vya habari vinanafasi kubwa sana katika kubadili maisha ya watu na vinatoa haki ya msingi ya kupata habari inayowezesha haki nyingine kupatikana .

“Hii sheria ya haki ya kupata taarifa haijaenda haraka sana isipokuwa tu watu hawakuitangaza wakati mchakato wake umeanza sababu mchakato wake umeanza mwaka 2014 na 2018 ilitaka kuletwa ikiwa na mambo mabaya zaidi imekuwa kwenye mchakato kwa muda mrefu” amesema Ndg Balile.

Aidha Mwenywkiti Mstaafu TEF Chief Teophil Makunga amesema waandishi wa habari ni muhimu sana katika kutetea na kusimamia demokrasia katika Nchi wanapofanya kazi yao kwa uhuru ndio demokrasia inakuwa huru zaidi kikao cha leo na vikao vingine vitasaidia katika kujenga uelewa wa Wandishi wa habari katika kufanya kazi.

“Ikumbukwe kwamba tumetoka mbali kwenye sheria ya vyombo vya habari kwa muda mrefu Nchi yetu ilikuwa inaongozwa na sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ilikuwa inavipengere vingi sana vilivyokuwa vinambana mwandishi wa habari kulingana na teknolojia iliyokuwa ya kipindi hiko” amesema Chief Makunga.

Chief Makunga amesema anaishukuru Serikali kwa kuliona hilo na imekubali kuongea na vyombo vya habari kurwkwbisha baadhi ya vipengere vya Sheria ambavyo wanafikiri vinawabana wandishi wa habari.

Sanjari na hayo Chief Makunga amesema mwandishi wa habari popote katika Nchi yeyote no mdau katika maendeleo ya Nchi na sio mpinzania katika maendeleo anapoewa nafasi ya kufanya kazi take kwa Uhuru unasaidia kusukuma maendeleo katika Nchi.

“Mimi naamini kabisa kwamba tunapoenda kuna mwanga unaonekana mbele wa kuwafanya waandishi wa habari waweze kufanya kazi yao vizuri na kwa uhuru ili waweze kuleta maendeleo kwa Nchi ” amesema Chief Makunga.

No

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!