Home Biashara TIGO WATOA MILIONI 140 KWA MAWAKALA WAO NCHI NZIMA.

TIGO WATOA MILIONI 140 KWA MAWAKALA WAO NCHI NZIMA.

Na Mwandishi Wetu.

 Kampuni ya Tigo Tanzania kupitia kampeni yake ya ‘Wakala Push Promotion’  imetoa zawadi kwa mawakala zaidi ya elf moja waliopo nchi nzima kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha wateja wa Tigo pesa wanapata huduma bora ili kukidhi mahitaji yao ya kifedha lakini pia kuchochea ukuaji wa uchumi kwa Mawakala wenyewe, jamii pamoja na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaa, Mkuu wa Huduma za kifedha kutoka Tigo pesa, Anjelica Pesha amesema  jumla ya washindi 1434 kutoka Tigo pesa wakala wanatarajia kujishindia takribani Milioni 140 baada ya kufikia malengo waliyoekewa;

Pia tutakua na washindi 10, wawili kutoka kila kanda zetu za Tigo,ambao watapokea 2m/- na 1m/-,jumla fedha zitakazo tolewa kwa washindi hawa ni 15m/-.”

Aidha Pesha amesema Promosheni hiyo ya kimkakati iliwapa mawakala katika kanda nne za Tigo ikiwemo Kanda ya Kaskazini, Kusini, Pwani,Zanzibar na Kanda ya Ziwa malengo maalum kulingana na ufanyaji wa shughuli zao za Tigo Pesa.

Aidha Pesha amesema Kama kampuni ya kidigitali wanahakikisha wanakuja na mikakati mbalimbali ambayo itawafanya mawakala nchi nzima kunufaika na huduma hiyo muhimu.

Kwa upande wake Zayd Muhidin Michuzi ambaye ni wakala wa Tigo pesa aliyekabidhiwa fedha Tshs. 2,000,000 kufuatia promosheni hiyo ya ‘Wakala Push Promotion’ amewashukuru Tigo kwa kuwawekea lengo na kufanikiwa kuwa mshindi lakini pia aliwaasa mawakala wengine wazidi kufanya miamala ili kuweza kuwa washindi;

“Nimeshinda kiasi cha Milioni mbili hivyo kwa mawakala wengine hasa wadogo wanaoanza kukua, wasikate tamaa waendelee kuongeza bidii, wafanye miamala kwasababu kadri wanavyofanya miamala hiyo biashara yao itazidi kukua na wao siku moja wataibuka kuwa washindi”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here