Home Kitaifa TBS YAWAFUNDA WATAALAMU WA MAABARA KAGERA.

TBS YAWAFUNDA WATAALAMU WA MAABARA KAGERA.

Mkuu wa wilaya Bukoba Mosses Machali akihutubia wakati wa ufunguzi wa semina ya wataalamu wa vipimo iliyoandaliwa na shirika la viwango Tanzania.
Sehemu ya washiriki wa semina wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa hotuba yake.

BUKOBA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendesha mafunzo kwa wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi kwa lengo la kuwapa ufahamu juu ya vifaa wanavyovitumia katika maeneo yao ya kazi na kuwataka  wataalamu hao kuitumia elimu hio kuhakikisha wanafanya upimaji wenye ubora.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo  hayo leo  September 09, 2022 mjini Bukoba, Mosses Machali Mkuu wa wilaya ya Bukoba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila, amelipongeza shirika la TBS kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yana umuhimu mkubwa kwa wataalamu wa Maabara.

Machali amesema kuwa elimu ya vipimo itaongeza ufanisi katika ufanyaji kazi na kutoa majibu yenye ubora kwa kuwa vifaa vinavyotumika kufanya vipimo tayari vimefanyiwa ugezi na kumpatia mpimwaji  uhakika wa majibu yake.

 Amewataka washiriki wa semina hiyo kuzingatia mafunzo wanayopewa ili kuwasaidia kwenye taasisi zao kufanya upimaji wenye ubora na kuendana na ushindani wa kimataifa na kuleta tija kwa wateja wao.

Baada ya mafunzo haya tunategemea mkatoe mafunzo kwa vitendo huko kwa wenzenu , nimearifiwa kuwa katika semina hii kuna wafanyakazi wa uzalishaji na upimaji katika viwanda, wataalamu wa maabara kutoka hospitali zetu, hivyo hatutegemei mkitoka hapa kuwepo manunguniko kwenye vipimo mnavyokwenda kundelea navyo” Amesema Machali.

Mhandisi Johanes Maganga Mkurugenzi wa upimaji na Ugezi(TBS) amesema kuwa semina hii itawapa ufahamu zaidi wataalamu kutumia vifaa wanavyovitumia katika maeneo yao ya kazi.

Maganga amesema kuwa wao kama TBS wanavifanyia vifaa vya upimaji ugezi ili viweze kusoma na kutoa majibu sahihi na baadae kutoa majibu ili kuthitisha ubora wa vipimo hivyo.

Ameongeza kuwa baada ya mafunzo hayo watawatembelea kwenye maeneo yao ya kazi kuona ni namna gani wanavitumia vifaa vyao, na kueleza kuwa  elimu ya vipimo inatakiwa kutolewa mara kwa mara.

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa semina hiyo, wamelishukuru shirika la TBS kwa mafunzo hayo ambapo wameeleza kuwa yatawasaidia kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Washiriki hao wamesema kuwa semina ya mara kwa  mara juu ya vipimo itawasaidia pia kujua ubora wa vifaa wanavyotumia na kuvifanyia marekebisho pale vitakapoonyesha tofauti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!