Home Kitaifa TANZANIA MBIONI MDUNDO WA ASILI WA KITAIFA

TANZANIA MBIONI MDUNDO WA ASILI WA KITAIFA

Na Magrethy Katengu.

Kamati ya Mdundo wa Kitaifa iliyoundwa hivi karibuni na Waziri Tamaduni Sanaa na Michezo Mohamedi Mchengrwa imesema inaendelea na mchakato wa ukusanyaji wa maoni katika Kanda zote nchi Ili kupata Mdundo wa Kitaifa utakaoutumika kitambulisho Tanzania .

Akizungumza Leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt Kedmon Mapana ambaye pia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amesema Kwa miaka mingi Wanamuzi wa Tanzania wamekuwa wakitumia mindundo ambayo haina asili ya Tanzania ikiwemo Piano hali inayopelakea kukosa fursa ya kualikwa kwenye majukwaa ya muziki ya kimataifa .

Wanamuziki wa Kitanzania wamekuwa wakikosa kualikwa kwenye matamasha ya muziki kutoka mataifa ya nje kutokana na nyimbo zao kukosa uhalisia wa mdundo wa asili kwani nyimbo nyingi wameigia mindundo ya nchi za Mangharibi” amesema Dkt Mapana

Hata hivyo Serikali inatarajia ndani ya miezi miwili iwe imeshakusanya maoni ya Watanzania kutoka makabila mbalimbali nchini huku wakishirikiana kamati hiyo yenye wajumbe 13 ikiwemo waandaaji,waimbaji nguli wa muziki hapa nchini ili kusaidia kufikia lengo waliokusudia

Sanjari na hayo amesema hatua hiyo ya ukusanyaji maoni walishaanza na Sasa wanafikia mbioni kuhitimisha hivyo Midundo inaweza ikawa zaidi ya miwili ikitegemeana na maoni ya Watanzania kwani kutumika kwakwe hakutokuwa na masharti mengi itaruhusiwa kutumika ndani na nje ili kusaidia kutangazika mbali zaidi .

Naye Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Mdundo wa Kitaifa ambaye ni Mtangazaji nguli wa TBC Masoud Masoud alisema Mdundo wa asili wa Kitaifa unaoandaliwa na Wizara ya Tamaduni,Sanaa na Michezo, utasaidia kumtambilisha mwanamuziki wa Kitanzania popote anapokwenda na kupata fursa zinazotokea ambazo zilikuwa zinawapita kutokana na kuiga Midundo ya mataiafa mengine .

Hii inasaidia Wanamuziki wa Kitanzania kutambulika kutokana na Mdundo wa asili wa Kitaifa, na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Burundi,Uganda,Kenya,Rwanda ha ta kule Nigeria na Kongo wana Midundo yao ya Kitaifa ambayo inawasaidi kupata mialiko yakuenda kushiriki kwenye majukwaa ya muziki katika mataifa ya ulaya na Marekani” amesisitiza Masoud.

Kamati hiyo ya Mdundo wa Taifa iliteuliwa mwezi Julai Mwaka huu na Waziri Mchengerwa ambapo Sasa imefanikiwa kukusanya vionjo vya makabila kutoka Kanda ya Kusini,Kanda ya Nyanda za juu kusini, Kanda ya Pwani,Zanzibar,huku ikitarajia kukamilisha katika Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa,na baada ya hapo kazi ya kuandaa Mdundo wa Kitaifa utaanza na kukamilika baada ya miezi miwili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!