Home Kimataifa TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MIKUTANO YA MABARAZA YA MAWAZIRI WA MAJI WA...

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MIKUTANO YA MABARAZA YA MAWAZIRI WA MAJI WA BONDE LA MTO NILE.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa heshima ya kuandaa mikutano ya mabaraza ya Mawaziri wa maji wa bonde la Mto Nile.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Leo 18 Agosti,2022,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Sekretarieti ya taasisi ya mpito ya Nile(Nile Basin Initiative-NBI) zimeanda Mikutano ya mabaraza ya Mawaziri wa Bonde la Mto Nile itakayofanyika Dar es Salaam Tanzania kuanzia tarehe 18-19 Agosti,2022.

Mhandisi Sanga amesema mikutano hiyo ni mkutano wa Baraza la Mawaziri wa maji wa ENSAP(Eastern Nile Counsil of Minister) utakaofanyika tarehe 18,.mkutano wa Baraza la Mawaziri wa maji wa Bonde la Mto Nile (Nile Council of Ministers – NILECOM) pamoja na mkutano wa baraza la Mawaziri wa maji wa ukanda wa maziwa makuu (Nile Equatorial Lakes Council of Ministers NELCOM) itakayofanyika tarehe 19 Agosti,2022.ambapo mikutano hiyo itatanguliwa na vikao vya kamati za wataalam kutoka nchi wanachama wa bonde la Mto Nile.

Aidha Mhandisi Sanga amesema mikutano hiyo inalenga kuendeleza ushirikiano wa Nchi wanachama wa bonde la Mto Nile katika kusimamia,kuendeleza na kutumia maji ya mto Nile kupitia mipango mikakati na programu za bonde kama vile mpango mkakati wa bonde la Mto Nile(Nile basin strategy 2017-2027) na programu ya miaka mitano ya bonde la Mto Nile(5-year basin wide program).

Pia Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Maji amefafanua kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kupewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mikutano hiyo pia itapokea uenyekiti wa baraza la Mawaziri wa maji wa bonde la Mto Nile kwa mwaka 2022/2023 kutoka nchi ya Jamhuri ya Sudani Kusini.

Bonde la Mto Nile, pamoja na Tanzania linahusisha nchi za Burundi,Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC, Misri, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudani Kusini,Sudani, na Uganda, nchi hizo zinashirikiana katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za maji za bonde la Mto Nile chini ya mwamvuli wa Taasisi ya mpito ya Nile Basin Initiative NBI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!