Home Kitaifa TANZANIA KUONDOKANA NA UPUNGUFU WA SUKARI 2023

TANZANIA KUONDOKANA NA UPUNGUFU WA SUKARI 2023

Tanzania iko mbioni kuondokana na changamoto ya upungufu wa sukari ya nyumbani na ya viwandani ifikapo 2023 mara baada ya ujenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi II kukamilika na kuanza kufanya kazi pamoja na upanuzi wa viwanda vingine vya sukari kukamilika.

Kiwanda cha Sukari Mkulazi II ambacho ujenzi wake umefikia 63% kiataanza kuzalisha sukari ya viwanda ili kuchangia kukidhi mahitaji katika ya tani 165,000 ya sukari ya viwandani inayoagizwa nje ya nchi kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) Oktoba 17, 2022 alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi II kilichopo Mbigiri Mkoani Morogoro kujionea jinsi ujenzi wa kiwanda hicho unaotarajiwa kukamilika Disemba 2022 unavyoendelea.

Aidha, Dkt. Kijaji amevipongeza viwanda vyote vya sukari ikiwemo Kiwanda cha Sukari Kagera, Mtibwa, Kilombero, TPC na Manyara vinavyoendelea na upanuzi kwa lengo la kuzalisha sukari inayotosheleza mahitaji ya ndani na kuweza kuuza nje ya nchi ifikapo 2025

Amesema iwapo viwanda vyote vilivyopo pamoja na viwanda vipya Ikiwemo Mkulazi II na Kasulu vinavyojengwa vikikamilika na kuanza uzalishaji vitaweza kukidhi mahitaji ya wastani wa tani 655,000 kwa mwaka nakuziba pengo la sukari kwa mwaka ambalo ni tani 42,000 lilioanza kupungua baada ya Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo uzalishaji wa tani 17,000 kwa mwaka.

Naye Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho Bw Selestine Sume amesema Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Kampuni Hodhi ya Mkulazi kwa ubia wa NSSF 96% na Jeshi la Magereza 4% kina uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka na kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 2,315 ambapo kwa sasa ni 958.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!