Home Kitaifa TANZANIA KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA

TANZANIA KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kufanya sensa ya uzalishaji viwanda kwa mwaka wa rejea 2023 (census of industrial production 2023) mwezi Machi 2025.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne tarehe 4 Februari 2025 jijini dodoma, ambapo amebainisha kuwa serikali ilifanya sensa ya mwisho ya viwanda mwaka 2013, na kwa mujibu wa sensa hiyo Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda 49,243.

Hata hivyo wakati wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 baadhi ya taarifa za viwanda zilizokusanywa zilibainisha kuwa Tanzania ilikuwa na jumla ya viwanda 69,106 ambapo viwanda vidogo sana vilikuwa 53,464, viwanda vidogo 13,367, viwanda vya kati 1,614, na viwanda vikubwa 661.

Aidha Dkt. Jafo amesema matokeo hayo yatatumika kupima utekelezaji wa mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano, programu za kikanda kama vile Dira ya Afrika Mashariki 2050.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!