Home Kitaifa SERIKALI KUENDELEA KUUNGA MKONO SEKTA BINAFSI – MBWASI

SERIKALI KUENDELEA KUUNGA MKONO SEKTA BINAFSI – MBWASI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais wake Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imejidhatiti kuziunga mkono sekta binafsi ikiwemo wafanyabiashara na wawekezaji nchini ikiwa ni kukuza uchumi pamoja na kufikia malengo ya Dira ya 2050 ambayo kwa asilimiq 70 inategemea sekta hizo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Aristides Mbwasi wakati wa Kongamano la Sheria za ushindani na wawekezaji Tanzania Mei 14,2026, Dar es salaam.

Mbwasi amesema ili kuweza kukuza Biashara na uwekezaji Serikali inaweka Mazingira mazuri ili iweze kunufaisha sekta hizo.

Amesema Tanzania inaendelea kushuhudia ukuaji mkubwa wa uchumi sambamba na kuongezeka kwa viwanda pamoja na ushiriki katika masoko ya kikanda na kimataifa, hali inayohitaji kuwepo kwa mifumo imara ya ushindani wa haki ili kuhakikisha maendeleo hayo yanaleta manufaa kwa wananchi wote.

Aidha ameongeza kuwa mkutano huo una tija kubwa kwa pande zote mbili kwa kubadilishana mawazo na kupeana ushauri ni namna watahakikisha Mazingira ya Biashara yatazingatia ushindani wenye haki.

Nae Kaimu Mkuu wa Tume ya Ushindani ((FCC) Khadija Ngasongwa amesema mkutano huo utaisaidia kuchechemua uchumi pamoja na kuweka Mazingira urahisi na wezeshi na uwekezaji ikiwa wa nje na ndani ya Tanzania kwani sekta ya ushindani inasaidia kuboresha Mazingira kwa mlaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!