Home Kitaifa SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA NI MHIMILI WA UCHUMI – KAMATI YA...

SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA NI MHIMILI WA UCHUMI – KAMATI YA BUNGE

Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, kupitia Mwenyekiti wake Mhe.Deodatus Mwanyika, ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi zake kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake, huku akizitaka kuongeza kasi ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayolenga kukuza uchumi wa taifa.

Mwanyika ametoa pongezi hizo wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za wizara kupitia taasisi zake za TBS, FCC, WMA na BRELA hiyo Mei 13,2026 Bungeni jijini Dodoma, amesema  juhudi zinazoendelea kufanywa zimeanza kuonyesha matokeo chanya katika kuimarisha mazingira ya biashara na uzalishaji nchini.

Aidha, Mwanyika ameiagiza wizara hiyo kuendelea kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya bidhaa bandia na hafifu zinazoingia sokoni, kwani zimekuwa zikisababisha hasara kwa wazalishaji wa ndani pamoja na kuhatarisha afya na usalama wa watumiaji ambapo hatua kali zinapaswa kuchukuliwa pamoja na vipimo visivyo sahihi katika biashara, hususan lumbesa, ambalo limekuwa likiwalalamikiwa na wananchi katika maeneo mbalimbali nchini na kuongeza kuwa matumizi ya vipimo visivyo rasmi

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo amesema wizara hiyo imepokea maelekezo na ushauri uliotolewa na Kamati hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa lengo la kuboresha huduma na kuongeza ufanisi katika sekta ya viwanda na biashara nchini.

Kwa upande wake, viongozi wa taasisi zilizochini ya  Wizara hiyo  akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Ashura Katunzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) Bi. Khadija Ngasongwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Alban Kihulla na Meneja wa Huduma za Biashara na Huduma wa Bw. Seka Kasera kwaniaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wameeleza kuwa wanaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha usimamizi wa bidhaa na huduma nchini, ikiwemo kufanya operesheni maalumu za ukaguzi wa bidhaa bandia na kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu matumizi sahihi ya vipimo vinavyotambulika kisheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!