Home Kitaifa TRA TANGA YAWANOA WANAWAKE WAFANYABIASHARA

TRA TANGA YAWANOA WANAWAKE WAFANYABIASHARA

Na Boniface Gideon, TANGA

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Tanga,imetoa Elimu ya mlipakodi pamoja na fursa mbalimbali zinazowazunguka Wanawake Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili kuwawezesha kutanua uelewa juu ya mifumo na Sheria za Kodi Nchini.

Akizungumza wakati wa kongamano la Wanawake na Kodi, Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Castro John,
Alisema TRA inatambua mchango wa Wanawake katika ulipaji wa Kodi Nchini nakwamba kwasasa Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika ulipaji wa Kodi,

“TRA inatambua mchango wa Wanawake katika ulipaji wa Kodi na kwasasa Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika ulipaji wa Kodi Nchini,hivyo naomba muendelee kuwa mstari wa mbele katika ulipaji wa Kodi ili tulijenge Taifa letu”Aliongeza Castro

Castro aliwataka Wanawake kuendelea kudumisha nidhamu ya ulipaji wa Kodi Nchini nakwamba Mamlaka hiyo ipo tayari wakati wowote kutoa msaada kwa mfanyabiashara anayepitia changamoto yoyote,

“Niwaombe muendelee kudumisha nidhamu ya ulipaji wa Kodi mliyonayo ili tuondoe usumbufu wowote unaoweza kujitokeza endapo mtu atakwepa kulipa Kodi,TRA ipo tayari wakati wowote kutoa msaada kwa mfanyabiashara anayepitia changamoto yoyote, niwaombe ukiwa na changamoto yoyote tuambie tukusaidia usikae nayo alafu baadae unakuja kulalamika” Alisisitiza Castro

Kwaupande wake,Naibu Katibu wa Jumuiya ya Nchini Wafanyabiashara, Ismail Masoud aliwataka watumishi wa TRA kuwasaidia kutoa Elimu Wafanyabiashara mkoani Tanga ili kuondoa kasoro nyingi zinazowakabili Wafanyabiashara,

“Niwaombe TRA iendelee kutoa Elimu ya mlipakodi ili changamoto za Wafanyabiashara hususani zinazotokana na Elimu ziishe, lakini pia kwasisi Wafanyabiashara,tuache janja janja zakukwepa Kodi, tunataka twende pamoja ili tuweze kufanikisha dira ya Taifa 2050” Alisisitiza Masoud

            MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!