Home Kitaifa WASIRA:CCM YALETA USAWA WA ELIMU KWA WANAWAKE NA WAVULANA

WASIRA:CCM YALETA USAWA WA ELIMU KWA WANAWAKE NA WAVULANA

Na Mwaandishi wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stiven Wasira, amesema chama hicho kimewakomboa wanawake kwa kuhakikisha wanapata elimu sawa na wavulana.

Akizungumza leo jijini Dodoma katika Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Wanawake wa CCM (UWT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Wasira alieleza kuwa, mwaka 1974 wasichana walikabiliwa na changamoto ya kutopatiwa elimu.

Amesema azimio la Musoma la mwaka huo, lililoongozwa na mwalimu Julius Nyerere, lililosisitiza umuhimu wa elimu kwa watoto wote, hata kama madarasa hayakuwepo.

“Tumeona wazi tangu kuzaliwa kwa CCM, idadi ya wanawake nchini kupata elimu imeongezeka kwa kiwango kikubwa hakika wanawake wa Tanzania wamekomboa,” amesema Wasira.

Na kuongeza kwamba,” Katika elimu ya juu, ufaulu wa wasichana umeongezeka kwa asilimia 62 yote ni kutokana na usawa ulioletwa na chama cha Mapinduzi, ” Amesema

Hata hivyo Wasira pia amemsifu Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya, hususan katika kuendeleza miradi ya kimkakati kama bwawa la Mwalimu Nyerere na mradi wa reli ya kisasa (SGR). “Hakika kazi inadendelea, Rais Dkt. Samia anafanya kwa vitendo,” amesema.

Amesisitiza kwamba uongozi wa Rais Samia umeleta maendeleo ya haraka katika sekta mbalimbali, ikiwemo uchumi, afya, elimu, na miundombinu.

Ameongeza kuwa CCM itaendelea kubaki madarakani kutokana na msimamo wake thabiti katika kulinda maadili na kusimamia maendeleo ya nchi.

Katika hatua nyingine, Wasira amesisitiza kuwa CCM kitaendelea kupinga mahusiano ya jinsia moja, akisema ni kinyume na maadili ya Kitanzania na hayakubaliki katika jamii.

Ameeleza kwamba chama kimejikita katika kulinda utamaduni, mila, na desturi za Watanzania, na hakitakubali shinikizo lolote kutoka nje linalopingana na misingi hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Mary Chatanda, amesema kwamba kupitia kongamano la kuazimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM, umoja huo unaunga mkono uteuzi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na uteuzi wa Dkt. Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza na Dkt. Hussein Mwinyi kama mgombea urais wa Zanzibar.

Chatanda ameeleza kuwa UWT itahakikisha inafanya kampeni za kitaalamu na zenye ufanisi wa hali ya juu, ili kuwahamasisha wanawake waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

“lengo ni kuhakikisha asilimia kubwa ya wanawake wanapiga kura kwa kishindo kwa ajili ya CCM katika uchaguzi wa mwaka 2025,” Amesema Chatanda

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!