Home Kitaifa TAASISI YA MWALIMU NYERERE YAKUTANISHA WADAU WA SIASA

TAASISI YA MWALIMU NYERERE YAKUTANISHA WADAU WA SIASA

Na Magreth Mbinga

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba amevitaka vyama vya siasa Nchini Tanzania wanapozungimzia mfumo wa vyama vingi wazungumzie mambo ya msingi ya kujenga na kuimarisha umoja wa Taifa.

Kauli hiyo ameitoa Septemba 20 wakati wa kufungua kikao cha kubadilishana ujuzi na uzoefu kilichoandaliwa na Taasisi ya Malimu Nyrere Foundation kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Tuache tabia ya vyama vya siasa baadhi ya vyama vinagawa Wananchi kama Nchi ikiwa huru Wananchi watakuwa huru na kama Nchi itakuwa na amani basi Wananchi watakuwa na amani” amesema Jaji Warioba.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara Mh Christina Mndeme amesema yeye kwa niaba ya Chama ameshiriki mkutano huo muhimu ilinkupata mawazo mbalimbali namna gani swala la umoja,amani na maendeleo linasimamiwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere takribani miaka 25 tangu imeanzishwa.

“Sisi sote tinaamini kwamba Nchi yetu ya Tanzania ambayo imepiga hatua kubwa sana katika swala la umoja,amani, maendeleo na hivo kuwa kioo na walimu wa Nchi zingine” amesema Mndeme.

Aidha Mdeme amesema katika uongozi wa Mwalimu Nyerere Nchi ya Tanzania imeshiriki katika kutafutia uhuru Nchi nyingine za Afrika kama Afrika ya kusini,Angola,Zambia,Msumbiji na nyingine mbalimbali.

“Aliyafanya haya sababu alitambua kwamba bila uhuru na umoja na haya akaunda Taasisi hii ambayo kwasasa unaongozwa na Mzee Joseph Butiku Leo hii tunaangalia namna gani viongozi wanatatua migogoro mbalimbaliya ndani na nje” .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!