Home Kitaifa TAASISI BINAFSI ZAOMBWA KUENDELEA KUUNGA MKONO SEKTA YA AFYA

TAASISI BINAFSI ZAOMBWA KUENDELEA KUUNGA MKONO SEKTA YA AFYA

Na Magrethy Katengu

Mstahiki Meya wa Jiji Dar es salaam Omary Kumbilamoto ameomba taasisi binafsi kuunga mkono Serikali kwa juhudu zao za kuendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ili kusaidia kuwapunguzia kutembea mwendo mrefu kufuata huduma

Ombi hilo amelitoa leo Dar es salaam katika hafla ya Ufunguzi wa Hospitali ya Royal Polyclinic Mnazi Mmoja ambapo amesema Serikali ya awamu ya sita kipaumbele chake ni kuboresha afya ya wananchi hivyo hospitali hiyo itatoa huduma kwa wananchi wote pasipo kubagua rangi,jinsia,dini,wala kabila

Sanjari na hayo amesema taasisi binafsi ikiwemo,taasisi za kiserikali dini,mtu binafsi zimekuwa zikisaidia jamii katika masula mbalimbali ikiwemo kusaidia Makundi Maalumu kwa kutoa Misaada huduma za kiafya hivyo Serikali anatambua juhudi zao na iko tayari kuwasaidia changamoto zinazowakabili kwani baadhi yao hawana maeneo ya kujenga hospitali wamepangisha majengo ambayo hata eneo la kuegesha magari hakuna.

“Sisi kama Jiji la Dar es Salaam tunafarijika kwa kuzindua hospitali hii hapa kwani itaipunguzia mzigo hospitali yetu ya Mnazi Mmoja. Tunashukuru kwa jambo hili ambalo mmelifanya,” amesema Mstahiki Meya Kumbilamoto.

Amesema kwamba Rais Samia Suluhu Hassani amekuwa akifanya jitihada kubwa kuboresha huduma za afya na tayari ameshatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Ujenzi wa vituo vikubwa vya Afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambavyo vitajengwa maeneo ya Mchikichini na Kiwalani.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Royal Polyclinic Bw.Ahmed Mohamed amesema katika kila mafanikio changamoto hazikosekani kwani hapo walipo wametoka mbali walianza na dispensari na wafanyakazi wawili na hadi hapo jambo la kumshukuru Mungu kwa kufikia hospitali na kuzalisha ajira zaidi ya 40

Mohamed amesema wamekuwa wakitoka huduma Zanzibar na kwamba katika Kituo hicho cha Dar es Salaam wamejipanga vilivyo katika kuwahudumia wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa ufanisi mkubwa kupitia madaktari

“Kituo hiki tumejipanga kuwahudumia wananchi Kwa ufanisi mkubwa kupitia Madaktari bingwa huduma ya Meno,maabara,Ultra Sound,Physiotherapy, dawa na vifaa Tiba kwa gharama fedha taslimu na bima ya afya hivyo wananchi wote tunawajali” alisema Bw.Ahmed

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!