Home Kitaifa MHE. SIMBACHAWENE, AHIMIZA WANANCHI WA KIBAKWE KUSHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI

MHE. SIMBACHAWENE, AHIMIZA WANANCHI WA KIBAKWE KUSHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa wananchi kujiandaa kwa zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuwa na kumbukumbu ya taarifa za watu waliolala katika makazi yako usiku wa kuamkia tarehe 23 mwezi 8 Mwaka 2022.

Sensa ya watu na makazi inasaidia serikali kupata idadi ya watu na kupanga mipango ya miradi ya maendeleo kulingana na uhitaji.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha mbuga jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Hata kama watu watatoka ni vizuri akabaki mtu mwenye kumbukumbuku za watu waliolala katika nyumba yake ili kupata takwimu sahihi alisema Waziri”

Naomba muendele kuwafahamisha wale ambao hawafahamu ili nao wawe na ufahamu na tuendelee kukumbushana kadri tunavyoelekea kwenye zoezi hili la sensa.

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi Million mia kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, barabara,

“Nitoe rai kwa watendaji kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ili ujenzi wa miundo mbinu uendane na thamani ya fedha iliyotolewa. Kuwe na Mtu maalumu anayesimamia ili aweze kuutolea taarifa sahihi inapohitajika alisema Waziri”

Awali katika salamu za shukrani Mwalimu Justine Maganga Mkuu wa shule ya sekondari Mbuga ameshukuru Waziri kwa miradi ya ujenzi wa madarasa matatu na madawati 150 pamoja na viti vyake, ukarabati wa jengo la maabara fizikia maabara ya fizikia na kemia pamoja vifaa vyake, jambo ambalo limewezesha wanafunzi kufanya mafunzo ya vitendo katika masomo hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!