Home Kitaifa SILAHA HARAMU 6208 ZATEKETEZWA JIJINI DAR ES SALAAM

SILAHA HARAMU 6208 ZATEKETEZWA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Magreth Mbinga

Mwaka 2022 jumla ya silaha 1220 zilikusanywa katika zoezi la usalimishaji na Mkoa wa Tanga umeongoza kwa kukusanya silaha nyingi ambapo zimekusanywa silaha 488 kufatiwa na Mkoa wa Tabora umekusanya silaha 247 na Mkoa wa Pwani 111.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini katika zoezi la uteketezaji wa silaha haramu 6208 katika uwanja wa silaha wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Hapa nilipongeze Jeshi la Polisi na wadau wake kufanikisha kusalimisha silaha hizi 6208 kama zisingepatikana zote hizi kungekuwa na usumbufu mkubwa sanakwa Wananchi wenzetu ikiwemo na sisi wenyewe “amesema Mhe. Sagini.

Pia Mhe. Sagini ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Usalama kufuatilia kujua sababu hasa kwa Mikoa hiyo mitatu na mingine inayoifatia kuwa na silaha nyingi,zinatoka wapi na nini chanzo pamoja na kuandaa mikakati ya kudhibiti silaha hizo.

Aidha Kamishna wa Jeshi la Polisi Libelatus Sabas ambae alikuwa anamuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Kamilius Wambura amesema zoezi hilo la ukusanyaji wa silaha haramu ulisimamiwa vizuri na kamati ya Ulinzi na Usalama,vikundi vya Ulinzi shirikishi , wenyeviti wa Serikali za Mitaa ,Madiwani pamoja na Viongozi wa Dini.

Hadi kufikia Oktoba 31,2022 jumla ya silaha 1220 zilikuwa zimesalimishwa kwa mchanganuo utuatao Bastola 18,magobole 1049,short gun 122,raifo 30 na AK 47(SMG) 1 ” amesema Kamishna Liberatus.

Sanjari na hayo Katibu Mtendaji wa REKSA Badrin Din amesema makubaliano yao na Nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni kudhibiti silaha ambazo zinamilikiwa kinyume cha Sheria.

Vilevile Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Ndg Herry James ambae alikuwa anamuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makala amesema dhamira ya Amirijeshi Mkuu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan ni kuona Nchi inakuwa salama wakati wote.

Uteketezaji wa silaha haramu ni moja ya njia ya kulifanya Taifa letu kuwa salama katika nyanja zote za kibiashara,Utalii na nyingine Kama hizo” amesema Ndugu Herry.

Ameendelea kwa kusema kuwa kupitia tukio hilo Wananchi watajengewa uelewa wa kutosha juu ya madhara ya silaha haramu katika jamii na kuweza kupata ujasiri wa kuweza kutoa taarifa za uhalifu kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama pale wanapobaini uzagaaji wa silaha haramu katika maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!