Home Kitaifa SERIKALI KUWALINDA WATOTO DHIDI YA VITENDO VYA KIKATILI

SERIKALI KUWALINDA WATOTO DHIDI YA VITENDO VYA KIKATILI

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kijiji cha Kisimba Katana Tarafa ya Kisiriri,katika shule ya msingi Kisimba.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Dc Mwenda amesema Iramba itamlinda mtoto na kumtengenezea mazingira wezeshi na bora ya kupata haki zake za Msingi.

DC Mwenda amewataka wazazi na walezi kutenga muda mahsusi wa kusemezana na watoto wao ili kugundua changamoto walizonazo ili waweze kuzitatua.

Mwenda amesema kulikuwa na Mila potofu katika jamii ambazo zilileta unyanyasaji kwa watoto kama ukeketaji, ambapo kwa sasa suala la ukeketaji limekwisha kabisa wilayani Iramba.

Wakati huohuo, DC Iramba ameeleza dhamira ya wilaya kuhakikisha shule za msingi na sekondari wanafunzi wote kupata chakula wawapo shuleni.

Ameongeza kuwa sera ya serikali inabainisha mtoto chini ya miaka mitano kupata huduma Bora ya afya sambamba na hilo amewataka wazazi na walezi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa ambayo gharama yake ni nafuu sana ili kuhakikisha watoto wanapata matibabu wakati wote.

Aidha, amewaomba Wananchi wote kujitokeza ifikapo tarehe 23 Agosti katika zoezi la Sensa na Makazi ili kuwezesha serikali kupanga mipango ya Maendeleo kwa ulinganifu kutokana na idadi ya watu na uhitaji wa Huduma.
Kauli mbiu ya kilele cha Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika inasema “Tuimarishe ulinzi wa mtoto, tokomeza ukatili dhidi yake. Jiandae kuhesabiwa”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!