Home Biashara EPZA YAONESHA NEEMA UWEKEZAJI ZAO LA KOROSHO KWA WAWEKEZAJI

EPZA YAONESHA NEEMA UWEKEZAJI ZAO LA KOROSHO KWA WAWEKEZAJI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje EPZA Charles Itembe akizungumza kwenye Mahojiano maalum na waandishi wa habari leo Julai 21,2022 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Revocatus Rashel (wa pili kushoto) akiwa katika jopo pamoja na vingozi wengine wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano maalumu unaoendeleza mahusiano kati ya nchi za Tanzania na Vietnam uliolenga kuitisha mitaji kutoka kwa wafanyabiashara wa Vietnam katika zao la korosho. (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje EPZA Charles Itembe (katikati) ni Balozi wa Vietnam Tanzania. Nguyen Nam Tien. kutoka kulia (wa kwanza) ni Norbert Kalembwe Meneja wa Bandari ya Mtwara, na (wapili kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Korosho Francis Alfred.

Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara Kwa kupunguza viwango vya kodi Ili kusaidia kuvutia Wawekezaji hasa katika zao la korosho na thamani yake kuongezeka .

Akizungumza Dar es salaam Mkurugenzi Mamlaka ya eneo maalumu la Uwekezaji na Mauzo Nje ya nchi nchini Tanzania (EPZA) Charles Itembe katika Programu ya ujio wa Wawekezaji kutoka Vetnamu na taasisi mbalimbali za kitanzania ikiwemo wawekezaji wa ndani katika zao la korosho lengo ni kuhakikisha wawekezaji wanahamasishwa kuwekeza katika zao hilo kuanzia Uzalishahi,ubanguaji,uchakataji katika viwanda na kuliongezea thamani Ili lipate masoko .

“Mwekezaji anayetaka kuwekeza EPZA anatakiwa awe na biashara yake isiwe chini ya dola laki tano na mwekezaji wa ndani si chini ya dola laki moja lakini kwa sababu tunawapenda wawekezaji viwango vya kikodi navyo akiteneza ajira angalau watu 50 anaweza kupata unafuu wa Kodi ambapo angetakiwa kulipa asilimia 30 hivyo hatolipa kabisa kwa kipindi cha miaka 10” alisema Itembe.

Hata hivyo amesema kuna uwekezaji mkubwa kwani tayari kuna viwanda vinavyofanya kazi vizuri hivyo taasisi imetenga maeneo yanayoweza kuwekezwa ambapo maeneo hayo ni pamoja na ikiwemo Dar es salaam,Bagamoyo,Mtwara,Tanga,Dodoma huku zao hilo pia likilimwa katika maeneo ikiwemo Ukanda wa Pwani kusini,kati,Dodoma,Singida na Mtwara.

Aidha kupitia Kuvutia Wawekezaji Serikali itaweza kuongeza ajira Kwa vijana,kina mama,na kutoa mitaji kutoka nje kwani kufanya hivyo ni fursa nzuri hivyo wawekezaji wa ndani na nje wanakaribishwa kuchangamkia fursa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!