Home Kitaifa RC AWAITA WADAU KUCHANGIA UJENZI KCMC MOYO

RC AWAITA WADAU KUCHANGIA UJENZI KCMC MOYO

Na Boniface Gideon, TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Batilda Burian , amewataka Wakazi wa Mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuchangia ujenzi wa Taasisi ya moyo KCMC inayoendelea kujengwa Jijini Moshi ambapo hadi sasa imefika 40% ya ujenzi wake.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati akiongoza harambee yakuchangia ujenzi wa Hospitali ya Moyo KCMC katika viwanja vya Tanga Beach resort,ambapo zaidi ya Sh.100Mil. zilichangwa na wadau wa Maendeleo huku wengine wakiahidi kuchangia zaidi.

Dkt.Batilda Alisisitiza kuwa Hospitali hiyo inatarajiwa kuhudumia zaidi wakazi wa Mikoa ya Kanda ya kaskazini Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara nakwamba tatizo la magonjwa ya moyo katika Kanda hiyo limekuwa kubwa,

“Kanda ya kaskazini inatoa asilimia 60 ya Wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI, hivyo endapo tukipata Hospitali hii itakwenda kusadia kupunguza idadi ya Wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI na wale wanaokwenda kutibiwa nje ya Nchi”Alisema Batilda

Dkt.Buriani alisema, mradi wa ujenzi wa Taasisi ya moyo KCMC inagharimu Sh.25Bil.ambapo mpaka sasa kiasi cha Bil.22 zimepatikana ambazo zimewezesha ujenzi kuendelea hivyo kumebakia Sh.3Bil.ambazo zitatumika kununua vifaa,

“Kwahiyo ndugu zangu,tumekuja hapa ili tuwe sehemu ya watu waliotoa mchango wa kuokoa maisha ya ndugu zetu, niwaombe tuendelee kuhamasishana kwa ndugu zetu ambao hawapo hapa, zoezi hili haliishii hapa tu bali ni endelevu hivyo kwayeyote atakayeguswa kuchangia basi afike ofisi za Mkuu wa Mkoa ” Alisisitiza Dkt.Burian

Kwaupande wake, Mkurugenzi wa KCMC Prof.Gilead Masenga alisema, kwasasa magonjwa yasiyoambukiza ndiyo yanayoongoza katika jamii,

“Pale Hospitali KCMC,kati ya Wagonjwa 10 wanaoletwa basi 8-9 niwagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza ambayo ikiwemo shinikizo la Damu,presha,kisukari nk.magonjwa yote haya huwa hayaambukizwi”Alisema Prof.Masenga

Prof.Masenga alisema Kutokana na idadi kubwa ya watu Wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza, Hospitali hiyo iliazimia kutoa huduma za kibingwa ili kuiwezesha jamii kupata huduma kwa haraka badala yakusubiri kwenye foleni ya muda mrefu katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI,

“Hospitali hii inatoa huduma za kibingwa kwa zaidi ya miaka 50,tunatarajia kuongeza huduma za kibingwa wa Moyo,hivyo tayari tumeshawaandaa wataalamu ambao tuliwapereka nje kwaajili ya masomo na sasa wapo tayari kwa kazi,kwa sasa tunasubiria kukamilika kwa ujenzi tu” Aliongeza Prof.Masenga

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!