Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili katika hafla ya utiaji saini mikataba kati ya TARURA na Mandarasi watakaotengeneza kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/23
Hafla hiyo inafanyika katika Ukumbi wa Jakaya kikwete Convention Centre Dodoma leo Agosti 14, 2022 na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa.