Home Kitaifa WIZARA KUANZISHA TANZANIA MADINI MARATHON MWAKA 2023

WIZARA KUANZISHA TANZANIA MADINI MARATHON MWAKA 2023

Na Steven Nyamiti-Shinyanga

Serikali kupitia Wizara ya Madini inatarajia kuanzisha mashindano ya mchezo wa mbio utakaojulikana kama Tanzania Madini Marathon ifikapo mwaka 2023 ili kuhamasisha watanzania kushiriki katika michezo maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa leo 14 Agosti,2022 na Waziri wa Madini Mhe.Dkt.Doto Biteko baada ya kushiriki Shinyanga Madini Marathon yaliyofanyika mkoani Shinyanga.

Aidha Dkt.Biteko amesema mwaka 2023 Serikali itafanya Tanzania Madini Marathon kuwa ya kitaifa kwa kuwashirikisha wadau wa sekta ya Madini na sekta nyingine ili kushiriki kwa pamoja.

Vilevile ametumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Sophia Mjema kwa kuandaa vizuri Shinyanga Madini Marathon ambayo imekuwa ya kwanza hapa nchini kuanzishwa.

Kwa upande mwingine Dkt.Biteko ametoa tuzo,medali na zawadi kwa washindi mbalimbali wa mbio fupi na ndefu,mbio za kukimbia na baiskeli pamoja na mashindano mengine ambao wamefanya vizuri na kumaliza mashindano.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Sophia Mjema ameipongeza Wizara ya Madini kwa kushirikiana pamoja katika shughuli hiyo na kusema kupitia mashindano hayo ya mbio imewezesha kuweka ukaribu wa Serikali na wananchi katika kufanya mazoezi ili kujenga afya.

Shinyanga Madini Marathon imekuwa ya kwanza kuanzishwa hapa nchini katika Mkoa wa Shinyanga na kuwakutanisha wadau mbalimbali kushiriki katika michezo kuanzia mbio za Km 21,Km 10, Km 5 na Km 2.5 na Michezo mingine mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!