Home Kitaifa RAIS SAMIA, KIONGOZI WA “FIELD” ANAENDELEA KUWEKA REKODI YA DHAHABU

RAIS SAMIA, KIONGOZI WA “FIELD” ANAENDELEA KUWEKA REKODI YA DHAHABU

Na Mwl Udadis, Njombe

Rais Samia anaendelea kupita katika kila Mkoa kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali na kutatua kero za wananchi. Licha ya kufanya ziara katika nchi mbalimbali zilizoleta tija kubwa, Rais hapumziki na kungojoea ripoti yuko “FIELD” katika Mikoa, Wilaya, Kata hadi Vijijiji.

Baadhi ya mambo yanayofanywa na Rais Samia katika ziara yake yanayovutia wananchi wengi;

1. Kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali katika ubora, muda wa utekelezaji, thamani ya miradi husika na namna inavyo saidia wananchi.

2. Kusikiliza maoni, ushauri, kero na hoja mbalimbali za wananchi moja kwa moja na kuzipatia ufumbuzi wa kina na kwa wakati.

3. Kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazolenga kuleta tija kwa wananchi wenyewe na kwa nchi yetu ikiwemo SENSA ya watu na makazi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

4. Kuimarisha misingi ya uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kutumikia watanzania katika nafasi mbalimbali za maamuzi.

5. Kujionea mafanikio ya kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kustawisha maisha ya kila mwananchi.

Uongozi wa Rais Samia ni kielelezo cha ubora unaohitajika katika kufanya mabadiliko ya kimaendeleo nchini. Watanzania tunazo sababu nyingi za kumpongeza kiongozi wetu huyu kwa kazi kubwa anayoifanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!