Home Biashara FCC; MAWAKALA FORODHA DHIBITINI BIDHAA BANDIA

FCC; MAWAKALA FORODHA DHIBITINI BIDHAA BANDIA

Tume ya Ushindani ya bidhaa(FCC) imewataka watendaji wa wakala wa forodha(TAFFA) kuhakikisha wanashirikiana Kwa pamoja kudhibiti bidhaa bandia kwani zimekuwa zikileta madhara Kwa watumiaji.

Agizo hilo amelitoa leo Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Tume ya ushindani ya bidhaa(FCC) Willium Erio katika ufunguzi wa semina fupi na Wafanyakazi wa TAFFA ambapo amesema bidhaa bandia hasa katika Mkoa wa Dar es salaam zimekuwa nyingi chanzo chake kikuu huingia kupitia bandari na wnaoziiruhusu ni miongoni mwao kwa kutolea faini.

Bandarini ndiko asilimia kubwa Wafanyabiashara wanakoingiza mizigo yao hivyo na bidhaa hizo bandia hupitia hapo na miongoni mwenu zinapokamatwa mnaingia kulipa faini Ili kuziruhusu zipite na zikishapita ile faini aliyoitoa hufidia kwa kupandisha bei hivyo mwananchi wa chini huumia kitwishwa mzigo ambao si wake “amesema Urio

“Mizigo inayoingia nchini mnaingiza nyie kwa niaba ya wateja wenu na mnawajua watu wenu ambao mnaofanya nao biashara muwe kinga ya kwanza kwa kufanya ukaguzi na muwe waaminifu ili kuzuia wimbi la bidhaa bandia” amesema Erio

Hata hivyo amesema kuna bidhaa bandia zimekuwa zikiingia kupitia bandari na zikikamatwa hatua za kisheria zinajulikana baada ya muda zinakutwa bidhaa zilezile tayari ziko sokoni zinauzwa hali hiyo imekithiri hivyo mawakala hamna budi kuliangalia hilo kwa jicho la tatu sababu zinapopita mikononi mwenu.

Nimekuwa nikifanya utafiti na kugundua ya kwamba nyie mawakala mnaoagiza bidhaa mmekuwa mkijua kinachoendelea isipokuwa hamtaki Wafanyabiashara wajue kuwa bidhaa zao ni bandia mnachofanya taratibu zote nyie za kulipa faini bila muhusika kujua tusaidiane” amesema

Hata hivyo amesema kuwa wakala amekuwa akilipa faini mzigo unaachiliwa kisha wanakwenda kwa mfanyabiashara kumwambia bidhaa imepanda bei na ushuru uko juu hivyo mfanyabiashara anakwenda kupandisha bei kwa walaji hivyo mzigo wote unakuwa juu ya mwananchi.

Wanachama wengine hawafahamu sheria hivyo kupitia kikao hiki kitasaidia kutekeleza majukumu yao vizuri kwa kufuata taratibu zilizowekwa Ili kusaidia kulinda Viwanda na wananchi.

Naye Alhaji Saudini Makamu wa rais Mawakala wa forodha chama cha TAFFA amesuma baadhi ya wamiliki wa Makampuni kuwa na Makampuni zaidi ya Moja Kwa kutumia majina ya watu wengine na tatizo hilo limekuwa kubwa hivyo tutashirikiana na Mamlaka ya mapato TRA kudhibiti hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!