Home Kitaifa PSPTB YASHAURIWA KUTOKUFUNGA OFISI ILIYOPO JIJINI DAR ES SALAAM

PSPTB YASHAURIWA KUTOKUFUNGA OFISI ILIYOPO JIJINI DAR ES SALAAM

Na Magreth Mbinga

Bodi ya manunuzi ya Umma PSPTB yashauriwa kuto kufunga ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuhamia rasmi Dodoma toka septemba 30,2022 ili kuweza kuwasaidia wateja wa Dar es salaam na mikoa inayoizunguka.

Hayo yamezungumzwa na Kamishna wa sera wa bodi ya manunuzi ya umma Ndg Fredrick Mwakibinga katika mahafali ya 11 ya bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Napenda kuwapongeza wahitimu wote ambao mutatunukiwa vyeti pamoja na shahada za umahili ila mfahamu kazi kubwa mmefanya ninaelewa vizuri hatua na changamoto mulizopitia leo munastahili pongezi ” amesema Ndg Mwakibinga.

Pia Mwakibinga amesema anawapongeza na kuwashukuru wahitimu wote kwa uvumilivu kwaajili ya kusubiri kuteuliwa kwa bodi ya wakurugenzi kama Wizara wanatambua changamoto iliyojitokeza na tayali imeshachukua hatua ili changamoto hiyo isijitokeze tena wakati mwengine.

Aidha Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi PSPTB Bw Jacob Kibona amesema mahafali hiyo ni ya 11 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi 2007 nakusema kuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha bodi matokeo yote ya mitihani ya bodi ni lazima yapitiwe na kuidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi.

Kwa bahati mbaya kuanzia septemba 2019 hadi novemba 2021 PSPTB haikuwa na bodi ya wakurugenzi baada ya iliyokuwepo awali kumaliza muda wake hali hii ilipelekea kutokufanyika kwa mahafali kwa miaka mitatu napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango hatimae bodi ya wakurugenzi imeteuliwa novemba 2021″ amesema Kibona.

Sanjari na hayo Mkurugenzi Mtendaji PSPTB Bw Godfred Mbanyi amewahasa wahitimu kufanya kazi kwa kufata maadili ya kitaaluma ili kulinda heshima ya fani yao na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasirimali za umma kwa manufaa ya Taifa .

Tunaposema maslahi muwe katika sekta binafsi au sekta ya umma wote munahitaji kufanya kazi kwa maadili makampuni binafsi tunahitaji yakue yatanuke yafanye biashara kubwa ili yaweze kulipa kodi Nchi iweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika jamii” amesema Mbanyi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!