Home Kitaifa RAIS SAMIA AAGIZA UJENZI OFISI ZA MACHINGA KILA MKOA KUANZA.

RAIS SAMIA AAGIZA UJENZI OFISI ZA MACHINGA KILA MKOA KUANZA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuandaa ramani maalum ya kujenga Ofisi za wafanyabiashara wadogo (Machinga) kwa kila Mkoa.

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo tarehe 15 Oktoba 2022 wakati akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Geita katika ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo.

Rais Samia amesema tayati ameshatoa kiasi cha Shilingi milioni kumi kila mkoa, fedha hiyo ipo TAMISEMI hivyo wahakikisha wanakamilisha zoezi hilo la kuandaa ramani kwa wakati na ujenzi wake uanze.

Aidha, Amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo rafiki ambayo machinga watapewa bure kwa ajili ya kujenga ofisi hizo.

Wakati TAMISEMI wanaandaa michoro, Wakuu wa Mikoa watengeze maeneo ambayo Wamachinga watapewa bure waweze kujenga ofisi zao na si maeneo ya kuwaficha uchochoroni “amesesetiza Rais Samia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!