Home Kitaifa NHC KUENDELEZA MIRADI YAKE ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA NYUMBA

NHC KUENDELEZA MIRADI YAKE ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA NYUMBA

Na Magrethy Katengu

Shirika la Nyumba la Taifa NHC limesema kwamba hivi karibuni litaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba unaojulikana kama Samia Housing Scheme ambao unalenga katika kujenga nyumba za makazi kwa ajili ya Watanzania wenye hali ya kati na chini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Nehemia Mchechu wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa uendelezaji milki Nchini Tanzania ambao ulifunguliwa na kufungwa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula Septemba 1-2 Jijini Dar es Salaam.

Mchechu amesema kuwa mradi huo wa nyumba za kuuza na kupangisha unakusudia kuenzi kazi nzuri anazofanya Rais Samia huku akibainisha kuwa NHC inatamani Watanzania wamkumbuke kwa miaka mingi ijayo.

Mchechu ameongeza kuwa asilimia 50 ya nyumba hizo zitajengwa Dar es Salaam, 20% Dodoma na Mikoa mingine zitajengwa kwa 30%.

Nyumba hizo zitaanza kujengwa mwezi huu wa Septemba eneo la Kawe Dar es Salaam (nyumba 500) na Medeli Jijini Dodoma (nyumba100). Mradi huu utakaotekelezwa kwa awamu utagharimu takriban Sh bilioni 466 sawa na dola za Kimarekani milioni 200″ amesema

Nyumba hizo zitawanufaisha Watanzania wengi kwasababu zitajengwa katikati ya majiji na kwamba zitajengwa katika viwanja ambavyo ni muhimu (very prime area)” ameongeza Mchechu

Mchechu ameongeza kuwa Katika mradi huo Shirika linatarajia kuajiri 26,000 na kulipa kodi mbalimbali za Serikali kiasi cha Sh bilioni 155.

Kuhusu Morocco Square amesema inakaribia kukamilika na ifikapo Novemba Majengo hayo yataanza kutumika na wateja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!