Na Mwandishi wetu Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe.George Simbachawene amepokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Bunge wa Saba kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Ramadhani Suleiman.
Akizungumza wakati wa kupokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. George Simbachawene tarehe 02/09/2022 amesema Serikali inaongozwa na sheria zinazotungwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo inaweza kutatua changamoto zote zinazogusa watu katika maswala ya sheria; kanuni, taratibu, mila na desturi zinazoongoza Serikali, alisema Waziri Simbachawene.”
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhani Suleiman amemshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kupokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba pamoja na majibu aliyoyatoa kwa Kamati ya Bunge.