Mwanafunzi FORTUNATUS Felician BUNDALA (17) amepata tuzo ya Jumuiya ya Madola kwa kutunukiwa tuzo ya Silver Award kutokana na kazi yake nzuri ya kitaaluma na ya ubunifu iliyoshindanishwa kati ya wanafunzi 26,300 kutoka nchi 60 za jumuiya ya madola.
Kijana huyu ambaye wakati anashiriki shindano hili alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha 6 (Masomo ya sayansi- PCB) katika Shule ya MT. Augustine- TAGASTE iliyopo Kimara jijini Dar Es Salaam katika wilaya ya Ubungo, na amemaliza shule mwaka huu 2022 kabla ya kujiunga na jeshi la kujenga taifa (JKT) katika kambi ya Kijeshi ya KIBITI kwa mafunzo ya kijeshii ya miezi mitatu kwa mujibu wa sheria. Kwa sasa Fortunatus Felician Bundala amedahiliwa chou kikuu cha Dar Es Salaam ( kampasi ya Mbeya) kwa taaluma ya udaktari ( Medical Doctor – MD).
Mashindano haya ya ‘’The Queen`s Commonwealth Essay Competition of Buckingham Palace’’ ni moja ya mashindano kongwe kwa wanafunzi vijana wa mashuleni kutoka nchi za Jumuiya ya Madola. Lengo la mashindano haya ni kuwatia moyo wanafunzi vijana kutoka nchi za jumuiya ya madola ili kuwajengea uwezo wa kujiamini katika kupaza sauti zao ili kuendeleza vipaji vyao.
Katika mpango huu washindani waligawanywa katika makundi rika mawili (Junior and senior categories). Kundi rika la kwanza (Junior category) ni wale walio chini ya ummri wa miaka 14 na kundirika la pili (senior category) ni kwa wale walio na umri wa miaka 17 hadi 18. Kijana huyu FORTUNATUS BUNDALA (miaka 17) alishiriki katika kundi rika la pili yaani (senior category).
Katika kuwaalika kwenye shindano hili la ubunifu ili kuondoa matatizo ya ulimwengu, waandaaji waliwataka washiriki kuandika hotuba zao “wakiwa kama viongozi wa nchi (Head of state) na kwamba wafikiri mkutano huo unafanyika nchini Rwanda. Mada yenyewe ilikuwa kama ifuatavyo
” Imagine that you are a Head of Government delivering a speech to your counterparts at the meeting in Rwanda. Write a speech to highlight what you believe should be a priority for collective action within the commonwealth.”
Mwanafunzi huyu Mtanzania, akivaa uhusika wa kama Mkuu wan chi, alijikita kuandika hotuba yake katika mada iliyohusu mfumo sahihi wa kutoa elimu katika nchi zinazoendelea. Fortunatus anaamini kuwa mfumo uliopo sasa haumpi mwanafunzi kujifunza kuwa mbunifu. Aidha Fortunatus Bundala katika hotuba yake hiyo kwa viongozi alisema mfumo wa elimu uliopo sasa haumsadii wala hauchochei elimu ya ubunifu na uvumbuzi kwa wanafunzi.
Akitolea mfano alisema kuwa, Mfumo wa sasa wa elimu unawakaririsha wanafunzi mambo yaliyogunduliwa huko zamani na kana kwamba baada ya uvumbuzi huo basi hakuna mwingine atakayezaliwa ili kugundua vitu vipya katika dunia ya leo, isipokuwa tu ni mawazo hayo hayo ya akina Sir ISAAC NEWTON, SIMON OHM, na wengineo, kitu ambacho kijana huyu anakikataa kabisa. Kijana anasisitiza mfumo wa elimu lazima ubadilishwe na kuwaaminisha wanafunzi wa sasa kuwa na wao wanayo nafasi ya kuleta mapinduzi mapya ya kisayansi katika dunia ya leo ambayo imetawaliwa na sayansi na teknonolojia. Alisema Kijana huyu Mtanzania katika hotuba yake hiyo.
katika andiko lake, kijana huyu wa Kitanzania, alitolea mfano katika sekta ya nishati, na akasema kuwa anaamini bado kuna mambo mengi ya kufanya katika sekta hii ambayo bado hayajafanyiwa utafiti na kuvumbuliwa. Alitolea mfano umeme unaotokana na RADI (lightning bolt.) kuwa umeme huu unaishia kupotea bure badala ya kunufaisha jamii ya hapa duniani ambayo kila kukicha inalalamika kuhusu upungufu wa nishati ya umeme.
Kijana huyu anakuja na mawazo ya kuvuna umeme unaotokana na rasilimali RADI ambayo Mungu huitoa kwa kadiri anapoona inafaa, lakini badala ya kutunufaisha umeme huu wa RADI unapotea bure na kuishia kuleta madhara na pengine hata maafa. Anasema kijana Fortunatus Felician Bundala (ambaye kwa sasa amedahiliwa kusoma kozi ya udaktari wa Binadamu (Medical Doctor) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kampasi ya Mbeya.
Katika hotuba yake hiyo Fortunatus Bundala alisema kuwa Umeme uliopo kwenye rasilimali RADI ni mwingi sana, (zipatazo TERAWATT 9). Hivyo ikitafutwa namna nzuri ya kuuvuna umeme huu utaleta manufaa na mapinduzi makubwa katika sekta ya nishati na hivyo kuendesha viwanda na shuguli zingine za binadamu kwa ufanisi zaidi. Lakini badala yake umeme huu umekuwa ukipotea bure na kuleta balaa kwa kuacha madhara ya uharibifu wa mali au hata vifo kwa wanadamu, mifugo, miti na mazingira.
Alisema kuwa leo hii dunia inahangaika kutafuta nishati, Maisha yamepanda kila kona ya dunia kwa sababu ya upungufu wa nishati, na sababu kubwa inayotolewa ni vita vya Urusi na Ukraine, Lakini kama umeme wa RADI ungeweza kuvunwa na kuwekwa stoo, mzozo wa Urusi na Ukraine isingekuwa sababu kubwa sana ya kulalamikia upungufu wa nishati. Hii haikubariki alisema kijana huyu, na kwamba yote haya yanatokana na mfumo mbaya wa elimu uliopo ambao watu huishia tu kusema hakuna wavumbuzi kama akina Sir Isaac NEWTON na wengine ambao kimsingi alikiri walifanya kazi kubwa, lakini anasema kuwa bado nafasi ya kuvumbua vitu vipya ipo kama mazingira ya kujifunzia yatabadilika.
Katika hotuba yake hiyo kijana huyu alisifia mfumo wa ujifunzaji kwa nchi za China na Marekani kuwa mfumo wan chi hizo ndiyo sahihi. Anasema kijana huyu mwanasayansi mchanga wa kitanzania katika hotoba yake kwa “viongozi wenzake aliyoitoa nchini Rwanda”
Kufuatia hotuba ya kijana huyu Mtanzania kupitia shindano hili la “The Queen’s Commonwealth Essay Competition (QCEC) 2022” majaji nchini Uingereza wakiongozwa na Dr. LINDA YUEH (Executive Chair, Royal Commonwealth Society) Dr. PAUL EDMONDSON (Chair, Senior judging Pannel) na IMTIAZ DHARKER (Chair,Junior Judging Pannel) na majaji wengine walitoa tuzo ya SILVER AWARD kwa kijana Fortunatus BUNDALA kutokana na andiko la hotuba yake na kumpongeza ambapo pia alitunukiwa cheti kutoka makao ya malkia Buckingham Palace ( ona kiambatisho No I)
Kijana Fortunatus akiwa tu ndiyo ana siku moja tangu ameripoti katika chou kiuu cha DSM tawi la Mbeya alipata ujumbe ufuatao kutoka Buckingham Palace nchini Uingereza unaosomeka kama ifuatavyo,
Dear Fortunatus BUNDALA,
“Thank you for participating in The Queen’s Commonwealth Essay Competition 2022 and for sharing your wonderful creativity and ideas with the Commonwealth family. We are delighted to inform you that your entry was given a Silver Award and am pleased to attach your printable award certificate“
“We encourage you to continue expressing your ideas through writing and harnessing the power that your voice holds within your immediate and global community. Remember, you can be the change you wish to see so please continue to write for a better world. Congratulations on your fantastic achievement and we very much look forward to receiving your entry next year!
With warm wishes,
The QCEC 2022 Team”.