Home Kitaifa Kocha wa makipa Simba akamatwa tuhuma dawa za kulevya

Kocha wa makipa Simba akamatwa tuhuma dawa za kulevya

Na Mercy Maimu

Mammlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watuhumiwa 11 akiwemo kocha wa makipa wa timu ya Simba Club, Muharami Sultan (40) anayetuhumiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin na bangi.

Hayo yameelezwa leo Novemba 15 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mbali na Muharami Sultani anayedaiwa kukutwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya heroin na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi, wengine waliotajwa ni pamoja na mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi seif, Said Matwiko mkazi Magole.

Wengine ni Maulid Mzungu maarufu mbonde (54) mkazi wa kisemvule na John John maarufu Chipanda (40) ambaye jukumu lake kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sport Academy. Wengine ni Rajabu Dhahabu (32) mkazi wa Tabata, Seleman Matola Said (24) mkazi wa Temeke Wailes, Hussein Pazi (24) na Ramadhani Chalamila (27).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!