Home Kitaifa MBUNGE GHATI CHOMETE AKABIDHI SIMU ZA MKONONI OFISI YA UWT MARA KWAAJILI...

MBUNGE GHATI CHOMETE AKABIDHI SIMU ZA MKONONI OFISI YA UWT MARA KWAAJILI YA USAJILI WA WANACHAMA KIDIGITALI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete amekabidhi simu za mkononi ofisi ya Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Mara.

Licha ya kukabidhi simu hizo ambazo zinakwenda kwenye ofisi zote za wilaya za UWT zilizopo mkoa wa Mara mbunge huyo ametoa kadi 1,500 za UWT na vifaa vingine kwaajili ya matumizi ya ofisi.

Akikabidhi simu na vifaa hivyo kwa Katibu wa UWT mkoa wa Mara Zaydani Mwamba amesema simu hizo zinakwenda kuwasaidia makatibu wa UWT wilaya kufanya usajili wa wanachama kidigitali.

Amesema CCM na jumuiya zake zinaendelea na zoezi muhimu la usajili wa wanachama na simu hizo zinakwenda kuisaidia UWT kwenye zoezi hilo.

Ghati amesema kwa kutambua zoezi la usajili na umuhimu wake ameamua kuishika mkono jumuiya hiyo ili iweze kutekeleza vyema majukumu yake.

Amesema licha ya jukumu la usajili zipo shughuli nyingine za jumuiya zinazofanywa ngazi ya wilaya na ndio kilichopelekea kutoa vifaa vingine vya ofisi.

Hii ni jumuiya yetu na tuna kila sababu ya kuishika mkono na ndio kilichopelekea leo kufika hapa kutoa simu pamoja na vifaa hivi vya ofisi”,amesema

Akipokea simu na vifaa hivyo Katibu wa UWT mkoa wa Mara Zaydani Mwamba amemshukuru mbunge huyo kwa kuona umuhimu wa usajili kidigitali na kutoa simu na vifaa hivyo vya ofisi.

Amesema sasa makatibu wa wilaya wanakwenda kutekeleza majukumu yao bila wasiwasi kutokana na kile walichokipokea toka kwa mbunge huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!