Home Kitaifa MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII.

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII.

By Mercy Maimu

Waziri wa Maliasiali na Utalii Balozi Dakta PINDI CHANA, amefungua maonyesho ya pili ya kimataifa ya karibu kusini katika viwanja vya kituo kikuu cha utalii kusini Kihesa Kilolo mkoani Iringa ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya kitalii vilivyo kusini.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza wakati wa kufungua maonyesho hayo, Waziri Balozi Dakta PINDI CHANA amesema kuwa ni wakati sasa wa kuvitembelea vivutio vya kitalii vilivyo kusini ili kuongeza watalii kutembelea na kuongeza pato la taifa.Aidha amesema kuwa serikali itatumia maonyesho ya kimataifa ya karibu kusini kama sehemu ya mkakati kutekeleza ilani ya CCM ya kufikisha watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025.

CHANA amesema kuwa kutokana na kampeni ya filamu ya Tanzania The Royal Tour ilifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kumesaidia kuongeza idadi ya watalii nchini kutoka watalii 922,692 mwaka 2019 hadi kufikia watalii 1,034,180.

Mikoa inayoshiriki maonyesho hayo ni mkoa wa Iringa, Morogoro, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Ruvu Lindi na Mtwara mikoa hiyo kwa kutumia maonyesho hayo itasaidia katika kutangaza vivutio vya utalii kusini mwa Tanzania.

CHANA ameongeza kuwa maonyesho hayo yakaribu kusini yenye kauli mbiu inayosema “UWEKEZAJI,KUSINI FAHARI YETU”ni jukwaa ambalo linawakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya utalii kwa lengo la kuuza bidhaa,kutafuta masoko pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara kwenye sekta mbalimbali za kitalii..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!