Home Michezo MANDOGA: KINESI ZITAPIGWA ZAIDI YA NGUMI NDOIGE

MANDOGA: KINESI ZITAPIGWA ZAIDI YA NGUMI NDOIGE

Na. Khadija Seif

Bondia wa Ngumi za kulipwa  Karim Mandoga aongoza zoezi la mabondia kupima Afya kuelekea pambano la Dar Boxing Derby Novemba 20,2022 Uwanja Wa Kinesi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Mara Baada Ya Zoezi La Upimaji Afya Kwenye Ukumbi Wa 361 Mwenge Dar es salaam  Mandoga amesema wanamasumbwi watarajie Kushuhudia vipaji vipya vikitoa Burudani ya aina yake kwenye pambano hilo ambalo atakuwepo kuhamasisha.

Nahamasisha mitaa yote ya Jijini Dar wajitokeze kwa wingi katika uwanja wa Kinesi kuona vipaji vipya na ngumi ya “Ndoige ” itaonekana pale kabla ya kwenda kwenye pambano Morogoro. “

Kwa Upande Wake Bondia Ismail Bokya atakayecheza Pambano kuu amesema Kiafya Yupo Vizuri Hivyo Mpinzani wake Ally Ngwando  atampiga kama mfuko kwenye pambano Hilo.

“Nishafanya mazoezi kwa ajili yake asinikimbie ubingwa nautaka,nataka nimpigie mpaka  mwenyewe aache.”

Hata hivyo boyka ameongeza kuwa atampiga kama mfuko Ngwando na hampangii atampiga raundi ipi na kumsisirizia ajiandae tu kwa kipigo japo hajaweza kujitokeza katika zoezi la kupima Afya kwa leo katika ukumbi wa 361 Mwenge Jijini Dar es salaam.

Daktari Wa Ngumi za Kulipwa Nchini Tanzania Khadija Hamis Mchenyi Amesema Ni kawaida Kwa Mabondia kabla Ya Kupanda Ulingoni Lazima Waangalie Afya Zao.

“Tumekuwa tuhakikisha mabondia kabla ya wiki mbili ya pambano tunahakikisha mabondia hao afya zao zinakuwa salama hivyo tunapima kisukari,homa ya ini,pamoja na virusi vya Ukimwi.”

Hata hivyo Khadija ameongeza kuwa tayari amefanya vipimo kwa mabondia 30 ambapo wanajiandaa kuwapa burudani ya ngumi kutoka kwa mabondia wenye vipaji vipya zaidi.

Mapambano 15 yakiwa Na vipaji Vipya vya Mabondia Wenye Mashabiki Mtaani yatapigwa Kwenye Pambano La Dar Boxing Derby Lenye Lengo La kupata vipaji Vipya Novemba 20,2022 Uwanja Wa Kinesi.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!